Wizara ya Afya mnaandaaje matamasha ya maombi na siyo kuweka mikakati ya kupima Corona?

Wizara ya Afya mnaandaaje matamasha ya maombi na siyo kuweka mikakati ya kupima Corona?

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Ni lazima tutambue nchi yetu inakibiliwa na adui mkubwa sana kuliko nduli Iddi Amin.

Leo nimesoma kwenye mitandao ya kijamii kuwa "WIZARA YA AFYA KWA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WA KIDINI NCHINI, IMEANDAA MAOMBI YA KITAIFA DHIDI YA MAAMBUKIZI YA KORONA YATAKAYOFANYIKA JUMATANO APRIL 22, 2020 VIWANJA VYA KARIMJEE"

Karimjee: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Aprili 22, 2020 atakuwa mgeni rasmi katika maombi ya kitaifa ya kuombea nchi dhidi ya janga la #COVIDー19 - JamiiForums

Taarifa hizi nimejiuliza mambo mengi nikakosa majibu lakini kubwa ni hivi wizara ya afya inao wakati sasa hivi wa kuandaa makongamano na matamasha ya maombi kweli?

Sijasema maombi yasifanyike, kama kuna mtanzania anaamini maombi yatatuvusha katika hili ruksa afanye lakini wataalamu wanaotuongoza katika hili janga la korona ni wizara ya afya na huku hatutegemei kusikia wataalamu hawa wakiibuka na hoja za tunguli, maombi wala kafara. HAWA KAZI YAO NI KUTUMIA UTAALAMU KUTUONGOZA NINI KIFANYIKE KUPAMBANA NA HILI.

Kama ataibuka mganga wa jadi akadai anaweza kutumia tunguli kuzuia korona na afanye yeye, kama ataibuka mtu na matambiko afanye yeye, kama ataibuka mtu na hoja ya maombi na fanye yeye.

Kila idara ibaki kwenye majukumu yake, idara ya waganga wa jadi ifanye yao huko huko na sio kuwashawishi wizara ya afya kutumia tunguli, idara ya maombi ya imani ifanye mambo yao huko huko na sio kushawishi wizara kufanya maombi. Nk.

Ili kila mmoja akiwa bize na kitengo chake kitengo kitakachoibua tiba sote tunafurahi lakini kuingiza shughuli za vitengo vingine katika shughuli hasa za wataalamu ni kuwadistruck wataalamu wasifanye kazi zao na kama hilo linalofanyika sio jibu na inaweza kutuletea majanga makubwa sana. Wapo wanaosema ukiacha jamii ikapata maambukizi kwa wingi na wakapona kwa wingi basi jamii inakuwa imejitengenezea kinga, Je kama tunachukua hili je tumejiuliza hili tunalitekeleza kwa gharama gani?

Ugonjwa huu unaonekana kutokuwastahi wazee na wenye magonjwa nyemelezi kama Kisukari, Pressure, moyo n.k. Hivyo kama tunaacha wengi waugue na wengi wapone ili tutengeneze kinga basi ni lazima tujue tutakuwa tumewatoa muhanga wazee wetu na wenye magonjwa nyemelezi.

Tunachokitegemea kutoka wizara ya Afya na serikali kwa ujumla ni kama haya yafuatayo

1. Mkakati wa kupima na kutambua wenye korona mapema na kuwa isolate ili kupunguza kasi ya maambukizi.

Katika hili swala la kupima bado ni changamoto, Juzi usiku wa tarehe 19/04/2020 katika kundi letu la watsapu la wana chuo tulielezwa mwenzetu tuliyesoma naye chuo kalazwa vihospitali vya mitaani. asubuhi ya tarehe 20/04/2020 tukaambiwa mwenzetu kafa na maiti haiwezi kutoka mpaka wapate majibu ya korona kama alikuwa anaumwa Korona. Leo Hii tarehe 21 / 04 /2020 nimeambiwa ndugu yangu alikuwa anafanya kazi tanesco tabata, kajisikia vibaya kazini akakimbizwa hospitali, kabla ya kupewa huduma yoyote akafariki na yeye pia kwenye msiba tunashindwa kwenda tukisubiri majibu kama ni korona au la.

Mtu anaumwa mitaani mpaka anakufa je ameambukiza wangapi? na je wanaweza kuwa traced wote au wataweka karantini familia yake tu. Maana yake kama ni vita upimaji wetu ni ule wa kupita kukusanya waliokufa na majeruhi basi na sio kutumia kupima kama ngao yetu ya vita kupingana na maambukizi.

Kupima kunakuwa zana ya kupigania vita iwapo tunaweza kufanya Haya.

kila mtu anayeeenda hospitali au vituo vya afya mwenye dalili moja wapo au kuhisiwa tu anachukuliwa sampo na kutumwa maabara huku anawani ya mgonjwa na namba za simu zikibaki kituo cha afya. Vituo vya afya vyote vipewe mafunzo ya jinsi ya kuhudumia wagonjwa wote kwa tahadhari na sio kuachwa na kituo kikipatikana kimemhudumia mgonjwa wa korona kinatengwa. wananchi wahimizwe kwenda kupima afya zao kwamba wakijitambua mapema na kufuata masharti ya afya watapona.

Mategemeo ni kupunguza kasi ya usambaaji wa Korona

2. Serikali imesema hatutafungia watu majumbani sawa lakini basi yale makundi ambayo yako kwenye hatari zaidi kama wenye magonjwa nyemelezi na wazee au wale ambao wako karibu na wenye magonjwa haya basi hawa hatuna namna bali hawa ni kuwaambia wakae majumbani tu. tuwaache vijana ambao wanaweza kupambana na ugonjwa huu waendelee kuzalisha na kulinda uchumi.

Kuwaacha watu walioko kwenye hatari zaidi kutavuruga mipango yetu ya kiuchumi. Mimi binafsi nimeacha kazi na kurudi nyumbani tangu mwanzoni mwa mwezi wa nne sababu sukari huwa inanisumbua na ninaamini nikinusurika katika hili nitapambana kuanza upya, lakini kesi nyingi ninazosikia mtu kaondoka ghafla na majibu yanasubiri vipimo vya korona ni wale wenye presha na sukari au magonjwa nyemelezi.

Sio watu wote wanaweza kuamua kuacha kazi kwa kuwa serikali haijaagiza, pengine mimi nimeweza kwa sababu niliwahi kuugua na kuona kama nimechungulia kaburi. Serikali ikitoa agizo katika hili itaweza kuwafanya hawa kutulia nyumbani bila msongo wa mawazo na tunaweza kuendelea kuchapa kazi
 
Lete pombe tunywe, maisha ndio haya haya, mtu unakua na Mali kibao halafu unakufa kwa Corona. Maisha hayana maaana
 
Huu ndiyo ujinga unaotufanya waafrika tusiendelee, ameomba Pope kule Vatican na Masheikh huko Saudi Arabia na HAKUNA kilichotokea. Mungu katupa akili ili tujisaidie wenyewe lakini wapi, tumekalia upuuzi wa dini wakati hazitusaidii chochote maishani mwetu. Tujitathimini jamani, hivi mpaka sasa hizi dini za kuletewa zimetupeleka wapi?
 
Shauku ya wengi wetu tunataka kujua watawala wetu wameweka mikakati gani pale ongezeko litakapo kuwa kubwa la waathirika naona kama tayari wanaojua kesho yao wameanza kujiwekea individual strategies ...ni muhimu kupata weekly updates juu ya huu ugonjwa ...Mungu tunampenda na tunamheshimu niwakati sasa wakufanya binadamu awezayo hii session ya maombi inaenda chukua picha mpya sasa
 
Ile Kamati ya Kitaifa ya kupambambana na COVID-19 ingekuja na mikakati na tathimini,au kupokea maoni ya wadau na wananchi kwa ujumla.

Hivi vyombo vya usafiri kama vingepewa sharti la kuwapa abiria barakoa kabla ya kupanda basi/daladala,na vyombo vingine kama boda boda

Je?, haiwezekani kufanya upimaji watu wengi kwa vitongoji na maeneo yaliyobainika kuwa na waathirika wa COVID-19,

Je?, maeneo hatarishi yamebainishwa na kuweka tahadhari na kinga,mfano masoko(watu ni wengi na upimaji haupo).

Yaani, hiyo michango inayotolewa inaenda kutatua changamoto na mikakati iliyo katika 'Kamati ya Kitaifa kupambana na COVID_19?!

Hiyo ni baadhi ya mitizamo yangu,tungeweza kuijadili au

Kuifanya Kamati ya 'COVID-19 na sekta ya afya waione kama kuna namna nyingine nzuri ya kuzuia kuenea kwa kasi kwa gonjwa hili.
 
Mara ooohhh....msichanganye dini na siasa lakini sasa hivi wanasiasa ndio wanajifanya wana dini kuliko hata viongozi wa dini. HUKU NI KUHADAA WANANCHI....
 
Back
Top Bottom