Wizara ya Afya, mulikeni madhaifu haya katika Hospitali ya Tumbi

Wizara ya Afya, mulikeni madhaifu haya katika Hospitali ya Tumbi

FURY BORN

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2020
Posts
638
Reaction score
1,150
Jana nimeenda hospital ya Tumbi kumpeleka ndugu yangu ambaye hayuko kwenye mfumo wa bima, baada ya kufungua faili kama taratibu mgonjwa wangu alitakiwa kuingia kwa Dr, nililipa gharama za yeye kuonana na Dr, shida ilianza pale alipohitaji kufanya vipimo ndipo nilipotakiwa kwenda kununua gloves kwa madai kuwa hospitali haina gloves.

Nimerudi na gloves naambiwa kipimo cha sukari hamna nikaelekezwa dispensary ya kwenda kufanya kipimo alafu nilurudishe majibu ikabidi niende.

Nimerudisha majibu Dr kamwandikia ndg yangu dawa, naenda phamarcy dawa zote nilizoandikiwa hakuna hata moja. Kifupi zaidi ya Dr hakuna kitu kingine nilichokipata Tumbi.

Hospital nika inakusanya tu hela ya registration na consultation fee.

Sijui kama hii imetokea bahati mbaya tu kwangu au ndivo ilivo na kama ndivyo ilivyo na hii ni hospitali ya hadhi ya Rufaa basi wizara ya afya na serikali kwa ujumla waliangalie.

Waziri afya mama Dr Gwajima pitia Tumbi, Dr Molel pitia Tumbi usiishie tu Mount Meru, Huruma nk. Njoo Tumbi tafadhari
 
Hili jina. La Tumbi limekaa kimazishi mazishi, nikisikia Hospitali ya tumbi kuna kua na kaharufu ka msiba hivi.
 
Aisee pole sana kwa hiyo ulienda kupiga picha na Dr tu!!?
 
Duuh sasa kama hospital tena yenye hadhi ya rufaa kukosa mpaka gloves si maajabu haya kama yake maajabu mengine!
 
Jana nimeenda hospital ya Tumbi kumpeleka ndg yangu ambaye hayuko kwenye mfumo wa bima, baada ya kufungua faili kama taratibu mgonjwa wangu alitakiwa kuingia kwa Dr, nililipa gaharama za yeye kuonana na Dr, shida ilianza pale alipohitaji kufanya vipimo ndipo nilipotakiwa kwenda kununua gloves kwa madai kuwa hospitali haina gloves, nimerudi na gloves naambiwa kipimo cha sukari hamna nikaelekezwa dispensary ya kwenda kufanya kipimo alafu nilurudishe majibu ikabidi niende. Nimerudisha majibu Dr kamwandikia ndg yangu dawa, naenda phamarcy dawa zote nilizoandikiwa hakuna hata moja. Kifupi zaidi ya Dr hakuna kitu kingine nilichokipata Tumbi. Hospital nika inakusanya tu hela ya registration na consultation fee.
Sijui kama hii imetokea bahati mbaya tu kwangu au ndivo ilivo na kama ndivyo ilivyo na hii ni hospitali ya hadhi ya Rufaa basi wizara ya afya na serikali kwa ujumla waliangalie. Waziri afya mama Dr Gwajima pitia Tumbi, Dr Molel pitia Tumbi usiishie tu Mount Meru, Huruma nk. Njoo Tumbi tafhadhari
Ukisikia tunanunua dawa na kupeleka kwenye hospital kwa hela zetu ujue ndiyo kama hivyo
 
nilipotakiwa kwenda kununua gloves kwa madai kuwa hospitali haina gloves,
nilikutana na hii kitu tar 22 mwezi huu kwenye hospitali ya wilaya, niliweka bandiko hapa kuna mtu akaniita MNAFIKI NA MSHENZI, afadhari wewe ulinunua nje ya hospitali mimi nilinunua gloves ambazo tayari zipo maabara na nikatakiwa kununua tena baada ya zile nilizonunua kuonekana zimetoboka. Imagine muuguzi ananipa gloves zimetoboka halafu anazikataa mwenyewe tena
 
Mzee wangu aliondoka hapo hapo kwa hadithi kama hizo...kanunue hiku, nenda kalete kile....(na tulikuwa na Bima_.. Kwa kweli Tumbi hapana. 😕
 
Back
Top Bottom