Kenya yathibitisha Visa vipya 4 vya Ebola. Jumla ya Wagonjwa yafikia 7

Kenya yathibitisha Visa vipya 4 vya Ebola. Jumla ya Wagonjwa yafikia 7

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
535
Reaction score
312
images-13.jpg

​
Kenya imethibitisha visa vinne vipya vya Ebola aina ya Bundibugyo, na kufanya jumla ya visa kufikia saba, akiwemo mgonjwa wa kwanza aliyefariki.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Afya, Patrick Amoth, wagonjwa hao ni ndugu wa karibu wa marehemu na wahudumu watatu wa afya waliomhudumia hospitalini.

Wizara ya Afya imesema wagonjwa wanapata matibabu, huku watu 128 kati ya 130 waliokuwa wamewasiliana na wagonjwa wakipatikana na kuwekwa karantini.

Serikali imesema hatari kwa umma bado ni ndogo, huku ikiwataka Wakenya kuripoti dalili kama homa, kutapika na kuharisha katika kituo cha afya kilicho karibu.

Soma Pia: Kenya yathibitisha mgonjwa wa tatu wa Ebola aina ya Bundibugyo

Wakenya wanaweza kupiga simu ya bure 719 kupata mwongozo zaidi kuhusu ugonjwa huo.

Source: The Star.co.ke

Updates

Kenya imethibitisha visa 8 vya Ebola hadi Oktoba 19, 2026, vikiwemo kifo kimoja. Kisa cha nane ni mwanaume mwenye umri wa miaka 49 aliyekuwa akifanya kazi katika kituo cha afya na aliwekwa karantini baada ya kubainika kuwa na maambukizi.

Mamlaka za afya zimewaweka karantini watu 128 kati ya 130 waliotambuliwa kuwa na mawasiliano na wagonjwa. Ugonjwa huo ni wa aina ya Bundibugyo, huku serikali ikiimarisha ufuatiliaji wa watu waliokutana na wagonjwa pamoja na uchunguzi wa afya mipakani.

Chanzo: Al Jazeera, ikinukuu taarifa za AFP, AP na Reuters.
 

Attachments

  • 2026-05-21T173317Z_2128550983_RC2ODLAMQTTF_RTRMADP_3_HEALTH-EBOLA-VACCINES-1320x740.jpg
    2026-05-21T173317Z_2128550983_RC2ODLAMQTTF_RTRMADP_3_HEALTH-EBOLA-VACCINES-1320x740.jpg
    228.2 KB · Views: 16
  • eastleighvoice-co-ke-2026-june-19-091610.webp
    eastleighvoice-co-ke-2026-june-19-091610.webp
    85.1 KB · Views: 21
Wizara ya Afya nchini Kenya imethibitisha kurekodiwa kwa visa vipya vinne vya virusi vya Ebola, na kufanya jumla ya wagonjwa nchini humo kufikia saba, ikiwa ni pamoja na kisa cha kwanza cha aliyefariki.

Nchi hiyo haikuwa imewahi kuripoti kisa chochote cha Ebola hadi Oktoba 6, kufuatia kifo cha mfanyabiashara Mkenya mwenye umri wa miaka 40 aliyekuwa akiishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Marehemu alisafiri kwa njia ya nchi kavu hadi Kampala, Uganda, kabla ya kupanda ndege kuelekea Nairobi mnamo Oktoba 3 na kufariki dunia tarehe 5 Oktoba akiwa kwenye matibabu.

IMG_3151.png


Miongoni mwa visa hivyo vipya ni ndugu wa kiume wa karibu wa marehemu aliyekuwa karantini tangu Oktoba 6, pamoja na wafanyakazi watatu wa afya (wanaume wawili wenye umri wa miaka 29 na 35, na mwanamke wa miaka 32) waliomhudumia mgonjwa huyo wa kwanza.

Wote walionyesha dalili za homa na kuwekwa karantini mara moja kabla ya vipimo kurejesha majibu chanya.

Visa vingine vilivyothibitishwa awali vinajumuisha mwanamke wa miaka 65 na mwanamume wa miaka 39, ambao wote ni ndugu wa mwathiriwa wa kwanza. Wizara imeeleza kuwa kati ya watu 130 waliochangamana na waathiriwa, watu 128 wamefuatiliwa na kuwekwa karantini, huku ikisisitiza kuwa hatari kwa umma bado ni ndogo kwani hakuna ushahidi wa maambukizi katika jamii.

Mlipuko huu unahusishwa na mlipuko wa 17 wa Ebola nchini DRC unaotokana na aina ya virusi vya Bundibugyo ambavyo havina chanjo wala matibabu maalum ambapo zaidi ya watu 9,066 wameambukizwa na 4,381 kufariki tangu Mei. Uganda pia ilirekodi visa 20 na vifo viwili kabla ya kutangazwa kuwa huru dhidi ya Ebola mnamo Agosti.

Source: France 24
 
Na kwanini chanjo wanapewa wauguzi wa ugonjwa huo pekee? Kwanini isiwe chanjo kama zilivyo chanjo zingine ili kila mtu apate?
 
Na kwanini chanjo wanapewa wauguzi wa ugonjwa huo pekee? Kwanini isiwe chanjo kama zilivyo chanjo zingine ili kila mtu apate?
Mbona wamesema virusi hivyo havina chanjo.
 
Kujipendekeza kwa wazungu sana mwishowe wanahangaika! Serikali ichukue hatua haraka kufunga mpaka na Kenya.
 
Kenya anajifanya ana Transparency Fulani Kwenye kuconduct mambo yake ya afya ila sidhani kama amefanya thorough Investigation Kuona future Impact yake kwa hicho anachofanya kuwafurahisha Donors kama US

Kenya kapewa mzigo mrefu Sana na US ajenge Center ya Kuhold wagonjwa suspected wa Ebola na US na Hii discussion iliwahi kuwa challenged na High court of Kenya ila kwa kuwa kasongo yeye linapokuja swala la hela basi hajali Ali force huo mpango kuwa implemented
 
Kenya anajifanya ana Transparency Fulani Kwenye kuconduct mambo yake ya afya ila sidhani kama amefanya thorough Investigation Kuona future Impact yake kwa hicho anachofanya kuwafurahisha Donors kama US

Kenya kapewa mzigo mrefu Sana na US ajenge Center ya Kuhold wagonjwa suspected wa Ebola na US na Hii discussion iliwahi kuwa challenged na High court of Kenya ila kwa kuwa kasongo yeye linapokuja swala la hela basi hajali Ali force huo mpango kuwa implemented
One tamu
 
Back
Top Bottom