Wizara ya Afya: Tumethubutu, Tumeweza, Tunazidi Kusonga Mbele

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,677
“Tumethubutu, Tumeweza, Tunazidi Kusonga Mbele “
“huduma sahihi kwa jamii ndiyo lengo letu”
“Wizara ya Afya na Ustawi Jamii”

...ndiyo kibwagizo (SLOGAN) inayokukaribisha kwenye lango kuu la Hospitali zetu za serikali.


...Kwakweli inasikitisha sana nilichokiona hospitali ya Amana ‘je hii ni haki kuwalaza wagonjwa wawiliwawili kwenye kitanda kimoja, tena bahati mbaya zaidi wengi wao wana magonjwa ya kuambukizana kwa hewa na ya ngozi.
Kwenye wodi #3 vitanda vyote vilikuwa na watu (wagonjwa) wawili wawili waliolala pamoja utafikiri ni wanandoa wenye mgogoro au waliochokana.

...yawezekana kabisa viongozi wa serikali hawatembelei hizi Hospitali !

Labda ni Hospitali ya Amana tu! Naomba kama kuna wadau wanaofahamu hospitali nyingine za Serikali zenye unafuu watujuze tafadhari... ili nimhamishe mgonjwa wangu.

.....Asanteni
 
… Na lini mpango na mikakati ya muda mrefu ya matibabu bure kwa wazee wasiojiweza na watoto chini ya miaka mitano kutibiwa bure – bilashaka hii ilikuwa danganya toto na imebaki kuwa porojo tu kwa serikali ya JK na Baraza lake la mawaziri!

Kwa muda mrefu tumekuwa Serikali imekuwa ikisema kuwa, ina mpango wa kuwasaidia wazee wasiojiweza kwa matibabu ya bure nakuwalipa pensheni ili waweze kujikimu kimaisha – kwanini wasiwe wakweli kuliko kuwadanganya wananchi?
Pamoja na ahadi hizo wazee na watoto wetu wameendelea kupoteza maisha kwa ugumu wa maisha, huku wengine wakiwa hawana ndugu au mtu wa kuwasaidia….
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…