Wizara ya Afya tunaomba kufahamishwa ugonjwa wa Monkeypox kabla haujazuka Tanzania

Wizara ya Afya tunaomba kufahamishwa ugonjwa wa Monkeypox kabla haujazuka Tanzania

chizcom

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2016
Posts
8,680
Reaction score
18,035
Kumeanza kuenea kwa habari kuhusu ugonjwa huu sehemu za mipaka nchi mbali mbali na hata huko USA na wagonjwa kupatikana.

Ugonjwa huu husababishwa na virusi vya nyani, na ni sehemu ya familia moja ya virusi kama tetekuwanga na ndui. Ni nadra sana nje ya Afrika, na CDC inasema virusi hivyo havitokei kiasili katika Mataifa.

--
Monkeypox is surging around the globe and now the rare virus has found its way inside our borders.

The first case of monkeypox in the United States this year was detected Tuesday when a Massachusetts man tested positive for the virus ... according to health officials.

The man recently traveled to Canada, according to the Massachusetts Department of Public Health, and the CDC confirmed his positive test result.

The MDPH says the man is hospitalized in good condition and poses no risk to the public, though they say they are working with the CDC on contact tracing.
 
IMG_6984.jpg
 
Kuna mtandao mmoja walipost hiyo habari hizo comments za wazungu ni full ubaguzi,kuita Africa nyani coz huyo mtu aliyepata alitokea Nigeria ukagundulika UK wakaanza kuita wa Africa monkeys ila chamoto walikipata anyways hivi walikosa majina mpaka wakaita ivo?

Wanataka ionekane huo ugonjwa umetoka Africa na ukute wametengeneza wao ili walete chanjo,,,chanjo za Covid big phama imepiga more than $500 billions wacha tuone but hiyo ni Chicken pox wamekuja kutuzuga tu watuletee machanjo yao!
 
Hawa jamaa hawajifunzi. Sasa wanakwenda kutafuta matatizo kwa kuwafuga nyani. Sisi huku tunao wengi tu, lakini tunahakikisha wanaishi porini na ni kosa kisheria kukutwa na nyara za Serikali kama hao nyani. Bahati nzuri kimeanzia kwao.

Kama ingekuwa toka nchi zetu za Afrika, nakuhakikishieni kesho tu wangetuwekea vizingiti kwenda kwao. Rejea Omacron COVID iliyogundulika Africa Kusini toka wasafiri wa Ulaya na jinsi nchi hiyo ilivyowekewa karantini. Kosa lao kugundua aina hiyo ya COVID!
 
Jana tu tumetoka kurudia chanjo ya polio kwa watoto chini ya 5yr nchi nzima kisa polio imezuka Malawi sijui, mzazi unamchanja mtoto huku una maswali mengi kichwani, haya madude yote mtoto anadungwa tangia anazaliwa, kweli hawa watu wanatujali sana au ndo biashara za watu nasi tunajitoa kafara tu,
Noma sana, ninachojiuliza hizi chanjo ambazo watoto wanachanjwa tangu utotoni je wazungu pia wanazipitia hivi hivi?
 
Mambo matano (5) ya kufahamu kuhusu HOMA YA NYANI (MONKEYPOX)

1. Virusi vinavyoeneza Homa ya Nyani vinatokana na familia ya orthopoxvirus ambavyo mara ya kwanza viligunduliwa kuathiri nyani . Virusi hivi vimegawanyika katika makundi makuu mawili (strains/clades): Vile vinavyopatikana Afrika ya kati (Congo basin Clade) na vile vinavyopatiaka Afrika ya magharibi (West African clade). Kati ya hivi viwili Congo Basin clade kinasadikika kuenea kwa haraka na kuleta dalili kali zaidi.

2.Ni ugonjwa unaoenea kutokana mgusano wa moja kwa moja (close skin contact) baina ya mtu na mtu aliyeathiriwa na huu ugonjwa au mtu na mnyama mwenye huu ugonjwa ,kwa njia ya hewa yaani (air droplets) ,majasho na mate (bodily fluids), pamoja na vitu ambavyo vina virusi hawa (virus-contaminated objects.)

3.Dalili za ugonjwa huu ni pamoja ya maumivu ya kichwa (headache),Upele (skin rash),homa(fever),maumivu ya mwili (body aches),ubaridi (chills) , kuvimba kwa lymph nodes (swollen lymph nodes) na uchovu (exhaustion) ;Dalili nyingi hushahabiana na zile za ndui (smallpox)

4. Ugonjwa huu huweza kutibiwa kwa chanjo lakini pia mpaka sasa ni dawa hii ya Tecovirimat ndio inashauriwa kutumiwa kwenye virusi vya jamii hii ya orthopoxviruses zaidi mgonjwa atapewa dawa kulingana na dalili na namna mwili wake unayopambana na maambukizi haya .

5.Ni muhimu kila mtu kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huu na kuwajibika kutoa taarifa pamoja na kwenda hospitali mara tu anapoona dalili za ugonjwa huu ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu .
 
Sisi huku ilikua inaitwa Chickenpox ilishatokomezwa zamani sana...

Hili la Monkeypox ni lao hao wazungu...
 
Kumeanza kuenea kwa habari kuhusu ugonjwa huu sehemu za mipaka nchi mbali mbali na hata huko USA na wagonjwa kupatikana.

Ugonjwa huu husababishwa na virusi vya nyani, na ni sehemu ya familia moja ya virusi kama tetekuwanga na ndui. Ni nadra sana nje ya Afrika, na CDC inasema virusi hivyo havitokei kiasili katika Mataifa.

--
Monkeypox is surging around the globe and now the rare virus has found its way inside our borders.

The first case of monkeypox in the United States this year was detected Tuesday when a Massachusetts man tested positive for the virus ... according to health officials.

The man recently traveled to Canada, according to the Massachusetts Department of Public Health, and the CDC confirmed his positive test result.

The MDPH says the man is hospitalized in good condition and poses no risk to the public, though they say they are working with the CDC on contact tracing.
Tafuta taarifa mkuu,wamekudanganya kwenye Covid,bado unategemea wakupe ukweli this time around,wake up and take care for your family and loved ones.No government can protect you.
 
Back
Top Bottom