DKT. MOLLEL: HATULAZIMISHI MTU LAKINI TUNATAMANI WOTE WAWEZE KUCHANJWA
Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema hawalazimishi mtu kupata chanjo ya #COVID-19 lakini wanatamani kila mmoja aweze kuchanjwa.
Amesema ili nchi iwe salama ni lazima 60% ya watu wawe wamepata chanjo.
Hadi sasa wamepata maombi kutoka taasisi nyingi nchini wakiomba chanjo jambo linalofanya chanjo zilizopo kutotosha.
Ameyasema hayo katika kipindi cha Clouds 360.