Wizara ya Afya: Uchunguzi uliofanywa mpaka sasa haujathibitisha uwepo wa virusi vya ugonjwa wa Marburg katika mkoa wa Kagera

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wizara ya Afya imepokea tetesi za uwepo wa ugonjwa wa Marburg katika Mkoa wa Kagera.

Kufuatia tetesi hizo, Wizara imechukua hatua kadhaa za haraka ikiwemo: kutuma timu ya wataalamu; kufanya uchunguzi wa suala hili; kuchukua sampuli na kufanya vipimo vya maabara. Mpaka leo, tarehe 15 Januari 2025, majibu ya uchunguzi wa kimaabara kutoka kwa wahisiwa wote waliochukuliwa sampuli hizo hayajathibitisha uwepo wa virusi vya Marburg.

Soma Pia: WHO: Watu nane wamefariki Kagera kwa ungojwa unahisiwa kuwa ni Marburg

Wizara inapenda kuwahakikishia wananchi pamoja na jumuiya ya kimataifa, likiwemo Shirika la Afya Duniani (World Health Organisation - WHO), kuwa imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa na itaendelea kutoa taarifa zaidi.


 
Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, amesema uchunguzi wa kimaabara haujathibitisha uwepo wa virusi vya Marburg katika Mkoa wa Kagera kufuatia tetesi zilizozuka kuhusu ugonjwa huo leo.

Waziri Mhagama amesema tayari wizara hiyo tayari imetuma timu ya wataalamu kufanya uchunguzi wa kina, kuchukua sampuli na kufanya vipimo vya maabara.

"Mpaka leo, tarehe 15 Januari 2025, majibu ya uchunguzi wa kimaabara kutoka kwa wahisiwa wote waliochukuliwa sampuli hizo hayajathibisha uwepo wa virusi vya Marburg," amesema Waziri Mhagama katika taarifa.

Hata hivyo, taarifa yake imesema Wizara imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa ugonjwa na kuahidi kutoa taarifa za mara kwa mara kwa wananchi na jumuiya ya kimataifa, ikiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO).
 

Attachments

  • 1736974825015.jpg
    108 KB · Views: 4
Sio Kenya tu hata ITV walitangaza, kinachonishinda ni kuwa serikali inaogopaga nini kusema ukweli kwa wananchi ili waelewe kuna janga flani wachukue tahadhari? Inamaana mpaka WHO kutangaza watakuwa hawajakurupuka
 

Wizara ya Afya imeutangazia umma kwamba uchunguzi wa kimaabara haujathibitisha uwepo wa virusi vya Marburg katika Mkoa wa Kagera kufuatia tetesi zilizozuka kuhusu ugonjwa huo leo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, wizara hiyo tayari imetuma timu ya wataalamu kufanya uchunguzi wa kina, kuchukua sampuli na kufanya vipimo vya maabara.

"Mpaka leo, tarehe 15 Januari 2025, majibu ya uchunguzi wa kimaabara kutoka kwa wahisiwa wote waliochukuliwa sampuli hizo hayajathibisha uwepo wa virusi vya Marburg," amesema Waziri Mhagama katika taarifa.

Hata hivyo, taarifa yake imesema Wizara imeimarisha mifumo ya ufuatiliaji wa ugonjwa na kuahidi kutoa taarifa za mara kwa mara kwa wananchi na jumuiya ya kimataifa, ikiwemo Shirika la Afya Duniani (WHO).

Wananchi wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari za kiafya na kuzingatia maelekezo kutoka kwa mamlaka husika.

Mashirika kadhaa ya habari ya kimataifa, leo yamelikariri WHO ikisema kwamba mlipuko unaoshukiwa kuwa wa virusi vya ugonjwa wa Marburg umewaua watu wanane katika mkoa wa Kagera.

Pia soma:
~
WHO: Watu nane wamefariki Kagera kwa ungojwa unahisiwa kuwa ni Marburg
~ Waziri wa Afya asema Hospitali Maalum ya Magonjwa ya Mlipuko kujengwa Kagera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…