Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,734
- 5,750
Kila mtu sasa hivi amechanganyikiwa, watu wanaishi kwa hofu maana elimu au taarifa kuhusu huu ugonjwa zinachanganya.
Mimi binafsi nilitarajia kuwa hata kila baada ya saa moja anakuja mtaalamu wa wizara ya afya na kutoa elimu juu ya huu ugonjwa kwenye Tv. Mfano mmoja tu ni kwenye kuvaa mask ni wazi kabisa WHO walitoa tamko kuwa mask ambazo zinaweza kuzuia huu ugonjwa ni mask aina ya N95 na Surgical mask.
Lakini sababu ya upungufu wakasema hata cloth mask zitumike japokuwa hawana uhakika kama zinazuia. Ila wakasisitiza Cloth mask atleast iwe na kitambaa kizito au wakati wa kushona ikunjwe mara mbili.
Mimi sijaona watalaamu wetu wakija kufafanua juu ya hili. Na mitaani kuna mask ambazo zinauzwa 500 au 1000 lakini unakuta kitambaa ni laini kabisa.
Pili ni wakati gani mask ivaliwe na eneo gani? Je kwa watoto na watu wazima wenye ugonjwa wa Athma? Wavae mask? Sijaona elimu yoyote juu ya hili.
Jambo lingine ni kuhusu taarifa na takwimu. Watu wanasema hali ni mbaya sana. Watu wanakufa kama upupu. Wizara ya afya haiweki uwazi kuwa kama ni kweli au vipi.
Pia ilitakiwa kitaalamu tuambiwe tuko katika stage gani? Maambukizi yanaingia? Yanasambaa? Yanapungua? Uzuri naibu waziri ni Daktari hivi anakosa hata muda wa nusu saa kuwa anafafanua haya mambo kwenye Tv?
Maana huku mitaani watu ni hofu tu. Tunaambiwa loaders na malori yanaenda kuzika watu kila siku. Kwa hiyo tunataka taarifa ambazo ni rasmi toka kwa vyombo husika.