Wizara ya Afya: Wazazi wazingatie uvaaji wa barakoa waendapo Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Dkt. Furaha Kyesi ambaye ni Afisa Mpango wa Taifa wa Chanjo ametoa rai kwa wazazi kuendelea kuwapeleka watoto wao kupata chanjo huku akiwakumbusha kuchukua tahadhari dhidi ya COVID19

> Huduma za chanjo nchini hazijasitishwa. Bado zinaendelea kutolewa kulingana na ratiba za watoto walizopangiwa na kulingana na umri wao hata hivyo jambo la msingi ni kila mmoja kuhakikisha anajikinga na corona kila anapompeleka mtoto.

> Kila mmoja anapaswa kuvaa barakoa. Jikinge ili uwakinge na wengine kwa sababu hapa hakuna anayejua mwenzake ametoka wapi, amekutana na nani hadi amefika hapa kwenye Zahanati

> Wazazi na walezi wanahimizwa kuzingatia kuvaa barakoa kila wanapowapeleka watoto wao Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kupatiwa huduma mbalimbali za kiafya ikiwamo zile za chanjo

 
Upvote 0
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…