Wizara ya Afya, yaanza kushindwa kusimamia Hospitali za Mikoa

Wizara ya Afya, yaanza kushindwa kusimamia Hospitali za Mikoa

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,327
Reaction score
4,624
Kuna taarifa kwamba Wizara ya Afya imeanza kushindwa kusimamia rasilimali watu zilizopo hospitali za mikoa.

Shida kubwa inatokana na mfumo wa Maafisa Utumishi wa Wizara kurundikana makao makuu ya Wizara.

Hivi karibuni, watumishi kadhaa wakihusisha madaktari waliajiriwa katika hospitali za mikoa na za rufaa zilizopo chini ya Wizara ya Afya, na hospitali za Wilaya zilizopo chini ya TAMISEMI. Jambo la kushangaza, watumishi walioajiriwa TAMISEMI wameshaanza kulipwa mishahara, huku wale walioko chini ya Wizara ya Afya wakiwa bado wanahangaika kukopeshwa mishahara katika taasisi walizopo.

Kuna uzembe fulani wa kitambo unafanyika katika Wizara ya Afya. Hivi hao maofisa Utumishi waliojazana makao makuu ya Wizara huwa wanafanya nini?
 
Back
Top Bottom