Wizara ya Ardhi itoe mrejesho wa mashamba pori ambayo Rais aliagiza wananchi wagawiwe

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Nimeona katika mitandao, SSH atakuwa mkoa wa Morogoro, ungependa uongozi wa mkoa huo utoe mrejesho gani kuhusu utendaji wa serikali?

Mimi naona apewe mrejesho kuhusu mashamba pori yaliyorudishwa kwa wananchi, kama walipewa hati, au laa, iwapo ilifanyika kazi ya kupanga matumizi bora ya ardhi, wangapi wamenufaika, kati yqo vijana wangapi, na wanawake wangapi. Pia uwiano wa wanufaika kati ya wakulima na wafugaji.

Weka la kwako hapa ambalo unataka Rais apewe mrejesho.

#waukae.

1722314302837.png
 
Usije kustaajabu takwimu utakazopewa. Ardhi ya morogoro sehemu kubwa ilishaliwa kwa urefu wa kamba 😏.
 
Wenyeviti wa vijiji husika kama wapo, wapewe fursa ya kusema, au wabunge, kuna sehemu nyaya zitagusana tu
 
Hapo kuna msafara wa magari zaidi ya 200 na kuna watu wametangulia kama wiki 2 na anachoenda kukifanya ni hakipo.
 
Rais ni taasisi, huwa haendi hivihivi, akienda kukagua mradi wa barabara, jua kwamba maofisa waandamizi ikulu wenye utaalamu wa mabarabara, wameshaenda kulikagua na kuangalia ubora wake, na kutoa mrejesho.

Kuna watu wa media, kuna watu wa "kuuchekecha" na kuu-scan mji, ili mambo yaliyompata Trump juzi yasitokee, security set up ya maeneo Rais atasimama, wanaongalia ratiba ngazi za mikoa na wilaya. Its a convoy, haiwezi kulingana na kakikundi kako kalikoenda kukutolea kishika uchumba au mahari
 
We ni mjinga sn, Rais na watu wake wa Ikulu wakitumia magari yasiyozidi 5, na wengine wakapanda kwenye mabasi hawatafika?
 
Nimekwambia, shughuli za Rais sio kama ile kamati yako ya kukutolea mahari walivyoenda na bajaji
 
Back
Top Bottom