chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Kliniki za ardhi, walau kwa kiasi fulani, hazitarajiwi kuwa suala la kudumu. Zitumike kutambua chanzo cha tatizo, na wizara iwasilishe andiko la kitaalamu kuhusu hasa kilichotufikisha hapo, na ikiwezekana lisomwe kwa watu wote, likiwa na mapendekezo ya suluhusho.
Mapendekezo hayo yarejeshwe kwenye jamii, ili jamii iangalie kama yanakidhi, na kama inawezekana jamii nayo ichangie, kwa kuwa ndio inaishi na kero hizo.
Mimi nazifananisha na jamii yenye wagonjwa wengi wa maleria, lakini iko bize kuwatibu, halafu wanarudi majumbami kwao kwenye mazalia ya mbu.
Kliniki zitumike kuonyesha viashiria vya mapungufu ya kisera, kiutendaji na kisheria, na jinsi ya kushughulikia tatizo hilo.
Hivyo ndivyo tunajenga mifumo imara ya kitaasisi.