Wizara ya Ardhi yawatakia heri wachezaji wake kuelekea SHIMIWI 2024

Wizara ya Ardhi yawatakia heri wachezaji wake kuelekea SHIMIWI 2024

Joined
May 14, 2024
Posts
94
Reaction score
75
Na.Mwihava GF,Dodoma

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Sheusi Mbuli kwa niaba ya Katibu Mkuu, amewatakia Heri wanamichezo wanakwenda kushiriki michuano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) inayotarajiwa kuanza Septemba 18, 2024 mkoani Morogoro.

Akizungumza na wanamichezo hao 18 Septemba 2024 wakati wa kikao kifupi Cha kuwaaga, amewataka kuipeperusha vyema bendera ya Wizara ya Ardhi, kuhakikisha wanazingatia nidhamu wakati Wote wa michezo na kufanya vyema katika Mashindano hayo.

Aidha Kwa upande wa Afisa michezo wa Wizara ya Ardhi nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi .Mwajabu Masimba amehaidi kupambana na kufanya vyema katika michezo hiyo.

Michuano ya SHIMIWI hushirikisha watumishi wa umma takribani 3000 kutoka maeneo mbalimbali nchini, inatarajiwa kuhitimishaa octoba 5,2024. Kauli Mbiu ya michuano hiyo ni Michezo huboresha utendaji Kazi, shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu.
 
Back
Top Bottom