Wizara ya elimu inaizika elimu ya tanzania rasmi baada ya kumaliza kuchimba kaburi lake.

Bunyu

Senior Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
119
Reaction score
32
Wizara ya Elimu Tanzania, imekuwa ikichimba kaburi la kuizikia elimu kwa muda mrefu sana! kwa kutosikiliza madai ya walimu, kutozipatia shule vitabu mujarabu vya kiada na ziada, kutokujenga maabara, kutojenga mabweni ya wanafunzi, kuwapeleka walimu katika vituo vyenye mazingira mabovu kabisa ya kufanya kazi utadhani ilikuwa lazima kila kijiji kijengewe shule! kuondoa nguvu ya mitihani ya kidato cha pili,kuruhusu Objective questions hadi katika hesabu kwa shule za msingi, na hili la juzi la BRN iliyokuja na aina mpya ya upangaji wa matokeo ya kidato cha nne yaliyowanufaisha wengi.

sasa katika kukamilisha maziko hayo, Wizara yetu hii "pendwa" inataka wanafunzi woote wa liomaliza form four 2013 na kupata ufaulu wa D katika masomo yake na yanatengeneza kombi, basi aende A LEVEL. What a shame! kwahiyo haitakuwa tena C This time eti ni D! MAKUBWA! Kama siyo kuizika kabisa elimu maana yake nini?
 
Sishangai hayo yanayotokea maana yanawanufaisha zaidi wale wanaotokea familia zinazojiweza na wanaosoma shule bora za binafsi.Katika uchunguzi wangu nimebain kua pamoja na BRN matokeo ya shule nyingi za kata huko vijijini yamebaki kua duni huku shule binafsi zikichanja mbuga.
 
mmh hiyo ya D mbona ndio naisikia kwako?? au upo wizarani mwenzetu.
 
D???? Wametangaza wapi maana hata mtu mwenye 4 ya 38 utakuta ana C 2 na D 3.
 
Kuna vikao vinavyoendelea kati ya Wizara na Wamiliki wa shule binafsi kwakuwa hawa ndiyo wanaleta nongwa juu ya jambo hilo!

kuna mengi yanayojadiliwa chini ya kapeti kwamba Wizara inataka hata wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule binafsi wapangiwe na wizara, yaani iwe kama inavyofanya TCU, sasa swali ada italipwaje? huo pia ni mjadala uliopo.

jambo lingine lililopo kmezani ni kurudisha system ya nusu kombi kwa wale wanaotaka kusomea ualimu, yaani ukimaliza kidato cha nne na umefaulu kwa ufaulu wao basi utaenda kusoma diploma ya ualimu kwa kusoma masomo mawili ya kufundishia na mengine ya education ambapo mwisho utapewa diploma.

Elimu ya Tanzania ni mambo mengi saana! it is so many things! and unstable! BRN
 
Embu tuache maneno mengi tutaumiza vichwa bure embu tusubiri mwongozo kutoka wizarani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…