Wizara ya Elimu ionyeshe uongozi katika kuchunguza masuala tata mashuleni

Wizara ya Elimu ionyeshe uongozi katika kuchunguza masuala tata mashuleni

Tikerra

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2008
Posts
1,702
Reaction score
147
Ni muda mrefu sasa matukio ya ajabu yamekuwa yakitokea katika mashule yetu.Jambo la kushangaza ni kwamba hakuna hatua madhubuti zinazo chukuliwa kutafuta chanzo cha matatizo hayo na hatimaye kuyatafutia ufumbuzi.Jana tarehe 10 September 2008, tukio lingine la watoto waliokuwa wanafanya mtihani wa darasa la saba limetokea huko Tabora.Katika hali isiyoeleweka watoto hao walianguka na kupoteza fahamu.Hii sio mara ya kwanza.Kuna mwelekeo kwamba watu wengine wanahusisha matukio haya na matendo ya ushirikina ,lakini mimi sina uhakika ingawa inawezekana.Ushauri wangu ni kwamba wataalamu wa mwili wa mwanadamu wahusishwe kikamilifu katika kutafuta suluhisho la kudumu la matatizo mbalimbali yanayotokea mashuleni.'Hormones' zote zinazohusika na 'human behaviour' ziangaliwe kwa undani.Kuna taarifa za kuaminika kwamba ipo mikakati ya makusudi ya kuharibu tabia za mwanadamu wa asili kupitia kwenye chanjo,madawa mbalimbali,vyakula,nguo nk..
 
Back
Top Bottom