WIZARA YA ELIMU na MAFUNZO yakanusha kuondoa Masomo ya DINI, KIARABU ktk MITIHANI ya TAIFA

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
by JOHN BUKUKU on OCTOBER 23, 2013 in JAMII



Na Faki Mjaka-MAELEZO - ZANZIBAR



Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema Masomo ya Dini,Kiarabu na Masomo mengine hajafutwa na yataendelea kusomeshwa na kufanyiwa Mitihani katika ngazi zote kama ilivyokuwa hapo awali.

Aidha imesema Wizara hiyo haijakubaliana na Waraka wa Elimu kutoka Tanzania Bara wa kuyafanya Masomo hayo kuwa ya hiari na hivyo yasichangie asilimia yoyote katika ufaulu wa Mtahiniwa.

Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Zanzibar Abdallah Mzee ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kwa lengo la kukanusha Taarifa zilizotolewa na baadhi ya Vyombo vya habari zilizodai kuwa Wizara hiyo imeondoa Mtaala wa Masomo ya Dini na Kiarabu kwenye Mitihani ya Taifa.

Amefahamisha kuwa Watendaji kutoka Wizara ya Elimu Tanzania Bara walikutana na Wenzao kutoka Zanzibar kwa lengo la kujadili Waraka wa Elimu waliokuja nao uliokuwa unataka kufanyike mambo mapya.

Mzee amebainisha kuwa katika Waraka huo Wenzao kutoka Bara walipendekeza kuwa Masomo ya Dini ya Kiislam, Dini ya Kikristo,Lugha ya Kiarabu,Kifaransa, Komputa, Mziki yawe ya Hiari kwa Mwanafunzi kuyasoma lakini pia yasisaidie ufaulu wowote katika viwango vya Madaraja ya Ufaulu.

“Waraka ulipendekeza Masomo hayo yakiwemo Dini na Kiarabu kuwa Optional na wala yasisaidie chochote katika kupandisha au kushusha Division ya Mtahiniwa” Alifafanua Mzee.

Aidha ilipendekezwa kuwa Utaratibu huo mpya uanzwe kufanyiwa kazi kwa Wanafunzi watakaoingia Kidato cha Kwanza mwakani ili ifikapo mwaka 2017 wanafunzi hao wautumie katika kidato cha nne.

Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu huyo alisema kuwa Watendaji wa Zanzibar waliupinga utaratibu huo kwa vile haukidhi matakwa ya Zanzibar.

“Watendaji wetu Waliupinga Waraka huo kwani hautufai na unatofautiana sana na Sisi kulingana na hoja zetu tulizotoa,lakini pia walikubali kuurudisha ili usiweze kufanyiwa kazi ” alisema Naibu Katibu Mkuu huyo.

Alisema kwa Zanzibar, Wizara ya Elimu inatoa Mchepuo wa Masomo ya Lugha katika Skuli tofauti ikiwemo Sekondari ya Kiponda hivyo itakuwa vigumu kufuata utaratibu huo.

Kuhusu Somo la Dini Mzee amesema Somo hilo kwa Zanzibar ni muhimu sana na nimiongoni mwa masomo yenye Walimu Wazuri wa ngazi za Stashahada hadi Udaktari-PHD ambapo ufundishwaji wake huanzia darasa la kwanza hadi Chuo Kikuu hivyo kubadili utaratibu isingewezekana.

Aidha amefahamisha kuwa katika dunia ya sasa Somo kama Komputa ni muhimu sana hivyo kulifanya halina ulazima ni kujirudisha nyuma kimaendeleo.

Amesema licha ya mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Wizara kwa upande wa Zanzibar na Bara lakini Wao hawakushirikishwa katika Uanzishwaji wa Waraka huo.

Katika hali ya kuliweka sawa jambo hilo Mawaziri wa Wizara hizo Ali Juma Shamhuna na Mwenzake wa Bara Shukuru Kawambwa wanatarajia kukutana kesho kulijadili jambo hilo.


IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
 
The best thing ni kuwaachia Wazanzibari kisiwa chao wafanye wayatakayo..... Tutaendeshwa puta hadi lini? For what? Let Zanzibar go!
 
Kwanini TZ Bara hawataki kuwashirikisha wenzao wa Zanzibar katika masuala yanayohusu Muungano? Suala la Katiba na hili la Elimu ni mifano michache.
 
Katika Nchi inayojinasibu kuwa haina dini,masomo ya dini ni ya nini huko mashuleni,kuwe na vipindi vya dini lkn sio masomo ya dini yaongeze ufaulu......nikishafaulu somo la dini naenda wapi,kuwa shekhe au padri?
 
Kwanini kodi yangu itumike kufundisha masomo ya DINI ya KIISLAMU NA KIKIRISTU? Kwanini Kodi yangu itumike kutunga na kusahihisha masomo ya DINI hizo?

kama kuna Wataalamu/waalimu waliobobea katika masomo hayo ya DINI kwanini wasianzishe SEMINARI zao na masomo hayo yakafundishwa huko kwa gharama zao!

STOP THIS MADNESS, THIS IS A SECULAR COUNTRY
 
Sasa watu wa waliunda mswada huu wakupendekeza kutolewa masomo ya dini na lugha ya kiarabu na kufanywa kwamba yawe masomo ya option yaani hayatakuwa yakiesabika kupandisha daraja la ufaulu je watu kweli wanawatakia wazanzibar kheri alafu vilevile wizara ya elimu ya zanzibar haikuusishwa kuunda mswada je hii ni haki
 
Sio lugha ya kiarabu tu...bali kiarabu na kifaransa.....
Hivi Zanzibar inapata kheri kama masomo ya dini na lugha ya kiarabu yakifundishwa mashuleni? Sidhani.

Masomo ya lugha aina mbalimbali yanaweza kufundishwa kwa makubaliano maalumu. Iwe kiarabu, kifaransa au kijerumani. Yanaweza kuwa kwenye mtaala rasmi au kuwa Option.

Binafsi sikubaliani na ufundishwaji wa masomo ya dini mashuleni, tena yafanyiwe mitihani na kutumika kupandsha madaraja. Ilihali hayana combination high school. I dont understand.

A self proclaimed secular state clinging into religion.
 
Ebana mbona combination ziko nyingi mfano KLA Na kitu chengine vyuoni xaxa iv kuna facult nyimg ambazo zinaitaj watu waliosoma ARABIC,ISLAMIC KNOWLEDGE ww unakataa coz BIBLE knowledge haina IMPACT yeyote ktk jamii kuliko islamic knowledge inamfanya mtua awe AWARE & CONSCIOUS kwa msingi huu BIBLE KNOWLEDGE ikifutwa hakuna hasara yeyote kwa jamii compared to ISLAMIC KNOWLEDGE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…