Wanitakiani
JF-Expert Member
- Apr 18, 2008
- 641
- 135
Nimefuatilia kwa makini matatizo ya wanafunzi wa Lutheran Junior Seminary na Mzumbe sekondari zote za Morogoro, nimebaini kuwa wanafunzi wana hoja. Migogoro hiyo imetokea kwa vipindi tofauti. Walianza wanafunzi wa Mzumbe Sekondari na madai yao ya miaka zaidi ya 7 bila kusikilizwa. Madai yao makuu ni ya kitaaluma, afya, uongozi na mazingira mabovu ya shule.
Kitaaluma, wanafunzi wanadai kuwa hawana waalimu ktk masomo ya biolojia na fizikia. Baadhi ya waalimu hufundisha topic moja kwa masaa 2-3 badala ya siku tatu! kiafya, hakuna mabafu na vyoo vya kutosha. Wanafunzi zaidi ya 150 hutumia mabafu 2 na tundu moja la choo na kusababisha milipuko ya magonjwa ya UTI, ngozi, homa ya matumbo na kuharisha. Mazingira, si salama kwa ulinzi na usalama wa wanafunzi. Hakuna security lights mwl. Mkuu amegoma kununua security lights kwa madai kuwa ni gharama kubwa (90,000/-) kitu kilichopelekea mwanafunzi mmoja kung'atwa na nyoka. Kukosekana kwa ulinzi, ambapo wanafunzi wamekuwa wakiibiwa mali zao na wezi kutoka nje ya shule. Wanafunzi wanapougua shule haiwajibiki kitu kinachopelekea wanafunzi kuchangishana ili kuhudumia wenzao wanapolazwa. Uongozi wa shule umegoma katakata kukaa na uongozi wa wanafunzi na kutatua kero zao za muda mrefu. Waalimu kutumia lugha ya matusi na kuwapiga ovyo wanafunzi bila sababu.
Baada ya vikao kushindikana Mwl. Mkuu aliwatisha wanafunzi na kuwaitia Polisi usiku wa manane, ambao waliwakamata baadhi yao na kufyatua risasi za moto. Wanafunzi walipoona hawasikilizwi, wamepigwa na polisi na risasi za moto waliondoka shuleni alfajiri kwenda kumtafuta Mkuu wa mkoa ili awasikilize kilio chao. Saa !! alfajiri walipofika Mindu walikutana na Polisi waliowazuia kuendelea na azma yao. Mkuu wa Mkoa hakuwepo Morogoro badala yake alimtuma RAS kuwasikiliza wanafunzi hao ambao walimtaka Mkuu wa mkoa kwa kuwa REO, RAS na uongozi umekuwa hauwasikilizi. Walitoka kwa amani wakarudishwa kwa amani shuleni. Matokeo yake Bodi ya shule ikawafukuza baadhi ya wanafunzi na Mwl. Mkuu kutoa maelezo ya uongo kwenye vyombo vya habari.
Issue ya Lutheran Junior Seminary nao Wanafunzi wana madai ya muda mrefu. Wanalalamikia kushuka kwa taaluma na kuwa na waalimu wasio na viwango. Mkuu wa shule hiyo amekuwa kwa muda mrefu hasikilizi kilio cha wanafunzi hao hadi walipotoka kuandamana kwa amani wakimtafuta mmiliki wa shule hiyo awasikilize. Kwa muda wa siku tatu wametaka kumuona Askofu Mkuu wa KKKT Bw. Malasusa na wanazuiwa na Polisi. Waalimu hawawasikilizi. wanajitokeza viongozi wa elimu mkoani hawana mbinu za kutatua migogoro hata kutoa muda wao kusikiliza hoja za wanafunzi wanakimbilia kufunga shule au kuwafukuza.
Nimeangalia ITV saa 2 usiku nimeumia sana! Wanafunzi wanafukuzwa waondoke shuleni saa 8 mchana hawana nauli, wamebeba masanduku hawajuwi wanaenda wapi na wengi wao wanatoka mikoani. Huu ni ukiukwaji wa haki za binadamu! wangeita wazazi shuleni kuwachukua watoto wao kuliko kuwatoa shuleni ghafla bila wazazi kufahamu. Nimeona ajabu aliyetoa amri hiyo alikuwa ni mwanamke, mama na mzazi. Nikajiuliza mwanamke asiyehurumia watoto wa wenzie anaweza kuongoza jamii? Maswali ya kujiuliza kwa migogoro ya wanafunzi wa shule hizo mbili:
1. Kwanini uongozi wa shule hautatui matatizo hadi yanafikia hatua ya kutovumilika?
2. Shule kama Mzumbe inayotoa wanafunzi bright kimasomo na ina vyanzo vya mapato, inashindwa nini kujenga hata matundu 2 ya vyoo inasubiri ruzuku toka serikalini?
3. Kwanini viongozi wanajenga utamaduni wa kuwafukuza wanafunzi bila kubaini kiini cha tatizo?
4. Kwanini hata pale wanafunzi wanapokuwa na hoja za msingi ktk madai yao hawasikilizwi? ingekuwa wanadai chai ya maziwa, mayai na chipps tungeshangaa,lkn wanadai kutatuliwa matatizo ya kitaaluma, kiafya na miundombinu ya shule ili wafanye vizuri zaidi na kuwa wataalamu wazuri siku zijazo. kwa hili serikali haioni umuhimu wa kuingilia kati?
Kama mzazi nimeumia sana na naiomba Serikali itatue matatizo sugu yanayochangia kushuka kwa elimu badala ya kufukuzana bila kutatua kiini cha tatizo.
Naomba radhi kwa uzi huu kuwa mrefu, kwa mzazi aliyeguswa kama mimi ataelewa.