pig man
JF-Expert Member
- Oct 14, 2013
- 292
- 319
Wadau bila shaka mnaendelea vizuri na mapambano ya kuliendeleza taifa katika nyanja mbali mbali, wakuu kama mtakumbuka serikali ilitoa tangazo la nafasi za mafunzo ya ualimu kwa ngazi zote mnamo mwezi april mwaka huu (2014) kipaumbele kikiwa ni kwa wahitimu wa kidato cha sita wenye daraja la kwanza hadi la tatu watakaoomba kujiunga na mafunzo ya ualimu kwa ngazi ya diploma na kwa masomo ya sayansi.
Tangazo pia lilitoa ahadi na commitment ya serikali ya kutoa ruzuku kwenye masomo kwa wanafunzi wenye ufaulu wa daraja la kwanza kidato cha sita watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo na pia kwa daraja la pili na la tatu kuwa watapewa mkopo, kama iyo haitoshi muda wa kozi hizi uliotangazwa na serikali ni miaka miwili, sasa cha kushanganza serikali kupitia Nacte walito majina ya ya waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbali mbali vya elimu ikiwemo Kleruu, Korongwe na kwingineko ila kinyume na ahadi na tangazo walilolitoa, sasa kozi zimekuwa tena sio miaka miwili kama walivyosema awali bali miaka mitatu na pia wamekaa kimya kwenye swala zima la udhamini na nyuo vinafunguliwa leo.
kwa kweli ijapokuwa serikali iliahidi ajira pindi wanachuo watakapomaliza mafunzo lakini hili la kubadilisha muda wa kozi na kukaa kimya kwenye swala zima la udhamini limetengeneza kasoro kubwa ya maamuzi ya serikali na hasa kuhusu utekelezaji wa ahadi zake.