Pre GE2025 Wizara ya Habari na Michezo pamoja na BASATA kuja na Tamasha la Kadansee la Mama Samia!

Pre GE2025 Wizara ya Habari na Michezo pamoja na BASATA kuja na Tamasha la Kadansee la Mama Samia!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Uchawa ni kansa ambayo tunaulea, siku vikibumbuluka tutajita sana!

=====

Kupitia ukurasa wake wa Insta@Gerson Msigwa ameandika haya;


Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) tunakuletea Tamasha la Muziki wa Dansi liitwalo KADANSEE LA MAMA SAMIA. Unakosaje?

Baada ya ukimya mrefu, sisi tunauanza mwaka 2025 kwa kurejesha heshima ya Muziki wa Dansi. Shughuli pevu kwa bendi zaidi ya 10 katika jukwaa moja itakuwa Februari 01, 2025 kuanzia saa 12:00 jioni pale LEADERS CLUB Dar es Salaam.

Hivi umepata picha ya hasira walizonazo Wazee wa Dansi, Wenye Dansi yao, wenye tungo za kumtoa nyoka pangoni baada ya kukosa jukwaa kwa muda mrefu wamepanga kurudije?

Sikia hii, KIINGILIO NI BUUUUREE!!! Yaani siku hii ni kula dansi mpaka chweee!!!!
 
Kadansee si neno toka kwa wakongo walete neno lao la kibongo!
 
Uchawa, kujipendekeza ni tatizo kubwa nchini, na kiongozi anaefurahia ahaya ana matatizo makubwa kichwani.
 
Back
Top Bottom