Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu.
Kwa hiyo kwenye hii nchi sasa hivi kila kitu kinapewa jina la Samia? Kwanini mnafanya kila kitu kwa tone ya Uchawa?
==============================================
Wakati nazunguka zunguka huko mtandaoni nimekutana na hii habari kwamba Wizara ya Katiba na Sheria kuwa wana program yao waliyoiita "Mama Samia Legal Aid Campaign" ambayo ina lengo la kutoa huduma ya msaada wa kisheria
Kampeni hiyo imezinduliwa rasmi Mkoani Iringa na itatekelezwa kwa siku 10 mfululizo, kuanzia leo hadi tarehe 19 Disemba 2024.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Ibrahim Ngwada, ameeleza kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuimarisha upatikanaji wa huduma za msaada wa kisheria na kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu sheria na haki za binadamu, hasa haki za wanawake na watoto.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Franklin Jasson Rwezimula, amesema kuwa kampeni hiyo ni ya kitaifa na inaendelea kutekelezwa kwa ushirikiano wa ngazi za kitaifa, kimkoa, na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
Soma pia:
Kesho, tarehe 11 Desemba 2024, kampeni hiyo itazinduliwa rasmi mkoani Mara, baada ya hapo, itazinduliwa mkoani Songwe tarehe 12 Desemba 2024, kisha mkoani Morogoro, Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa wananchi wa mikoa yote ya Tanzania wanapata huduma za msaada wa kisheria kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

- Zawadi, Misaada na Michango Iliyotolewa na Rais Samia kwa Watu na Taasisi Mbalimbali Tangu Alipoingia Madarakani
- Generation Samia kuanza na Jogging kubwa ya historia Dodoma