Wizara ya Madini yaendelea kutoa darasa la kutumia mfumo wa ‘Monorope System Winchi’ kutoa udongo kwenye mgodi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kwa kushirikiana na Kampuni ya Kidee Mining Ltd wanaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo na wa kati wa madini wanaotembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, namna ya kutumia mfumo wa ‘Monorope System Winchi’

Mfumo huo ni wa kutoa udongo kwenye mgodi kwa kutumia vifaa maalum ambavyo vitamuwezesha mchimbaji kutoa tani 10 hadi tani 13 kwa saa moja tofauti na mfumo wa kizamani wa kutumia ndoo na viroba kutoa udongo mgodini.
WhatsApp Image 2024-08-05 at 15.07.19_196a4aa5.jpg

WhatsApp Image 2024-08-05 at 15.07.20_b2ff6038.jpg
Akizungumza Mkurugenzi wa Kampuni ya Kidee Mining (T) Limited, Fey Kidee amesema mfumo huo wa zamani mchimbaji anatoa udongo kilo 60 kwa siku na kumuongezea mzigo mkubwa wa kazi tofauti na mfumo huo wa Monorope ambao unarahisisha.

“Tumekubaliana na Tume ya Madini kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo na wa kati nchi nzima ili waufahamu huu mfumo wa kisasa uliopo na kuachana na mfumo wa zamani wa kutumia ndoo na viroba,”amesema Kidee.
WhatsApp Image 2024-08-05 at 15.07.18_8e7019bd.jpg

WhatsApp Image 2024-08-05 at 16.01.36_3dca5613.jpg

WhatsApp Image 2024-08-05 at 16.01.36_48d6d297.jpg
Aidha, amesema mfumo huo wa kisasa unasaidia kuongeza mapato kwa Serikali na mchimbaji mmoja mmoja ikiwemo kuokoa muda.

Kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan alizozifanya kwenye Sekta ya Madini, tumeweza kuinuka wachimbaji kutoka uchimbaji mdogo hadi kufikia uchimbaji wa kati hivyo ni muhimu sisi kama Kidee Mining kuunga mkono juhudi za Rais Samia kwa kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo tukishirikiana na Tume ya Madini ili nao wapande kutoka uchimbaji mdogo kuja uchimbaji wa kati,”amesisitiza.

Kidee Mining (T) Limited inayojihusisha na uchimbaji madini na uuzaji na usambazaji wa vifaa vya uchimbaji madini, uchimbaji wa kisasa, ilianzishwa mwaka 2000 ambapo mpango ni kutanua zaidi matawi yake kwa kuongeza migodi na kutengeneza ajira nyingi kwa watanzania.

Soma pia: Tume ya Madini yawashauri wachimbaji wadogo kutumia zege kwenye kingo za miamba badala ya magogo
 
Wizara ya Madini kupitia Tume ya Madini kwa kushirikiana na Kampuni ya Kidee Mining Ltd wanaendelea kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo na wa kati wa madini wanaotembelea Banda la Tume ya Madini katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, namna ya kutumia mfumo wa ‘Monorope System Winchi’

Mfumo huo ni wa kutoa udongo kwenye mgodi kwa kutumia vifaa maalum ambavyo vitamuwezesha mchimbaji kutoa tani 10 hadi tani 13 kwa saa moja tofauti na mfumo wa kizamani wa kutumia ndoo na viroba kutoa udongo mgodini.
Akizungumza Mkurugenzi wa Kampuni ya Kidee Mining (T) Limited, Fey Kidee amesema mfumo huo wa zamani mchimbaji anatoa udongo kilo 60 kwa siku na kumuongezea mzigo mkubwa wa kazi tofauti na mfumo huo wa Monorope ambao unarahisisha.

“Tumekubaliana na Tume ya Madini kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo na wa kati nchi nzima ili waufahamu huu mfumo wa kisasa uliopo na kuachana na mfumo wa zamani wa kutumia ndoo na viroba,”amesema Kidee.
Aidha, amesema mfumo huo wa kisasa unasaidia kuongeza mapato kwa Serikali na mchimbaji mmoja mmoja ikiwemo kuokoa muda.

Kutokana na jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan alizozifanya kwenye Sekta ya Madini, tumeweza kuinuka wachimbaji kutoka uchimbaji mdogo hadi kufikia uchimbaji wa kati hivyo ni muhimu sisi kama Kidee Mining kuunga mkono juhudi za Rais Samia kwa kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo tukishirikiana na Tume ya Madini ili nao wapande kutoka uchimbaji mdogo kuja uchimbaji wa kati,”amesisitiza.

Kidee Mining (T) Limited inayojihusisha na uchimbaji madini na uuzaji na usambazaji wa vifaa vya uchimbaji madini, uchimbaji wa kisasa, ilianzishwa mwaka 2000 ambapo mpango ni kutanua zaidi matawi yake kwa kuongeza migodi na kutengeneza ajira nyingi kwa watanzania.
Aisee huko huko Nzuguni kuna machimbo ya dhahabu!Nenda uje na mrejesho wa hicho kifaa.
 
Back
Top Bottom