Wizara ya maji yanufaika na ziara ya Rais Samia Korea

Wizara ya maji yanufaika na ziara ya Rais Samia Korea

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
WIZARA YA MAJI YANUFAIKA NA ZIARA YA RAIS SAMIA KOREA

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema ziara iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan nchini Korea Kusini imetengeneza mahusiano mazuri na kuchangia kupatikana kwa fedha kwa ajili ya mradi mikubwa wa maji safi na usafi wa mazingira.

Akizungumza leo Disemba 16,2024 baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Ujenzi wa Mradi wa Mfumo wa Kutibu Majitaka Katika Jiji la Dar Es Salaam ikiwa ni siku chache baada ya Ziara ya Waziri Aweso na timu nzima ya sekta ya Maji Nchini Korea Kusini.
Aidha Waziri Aweso amesema "baada ya kupata nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya ziara ya Korea Kusini kwa muda mfupi sana baada ya kumaliza na mimi nimepata nafasi hivi karibuni kwenda haijafika hata wiki tumepata zaidi ya dola za kimarekani zaidi ya milioni 240 kwa ajili ya uwekezaji kwenye maji taka”

Ameongeza kuwa hiyo inathibitisha mahusiano mazuri na urafiki wa thamani uliopo baina ya nchi hizi mbili ikichangiwa na ziara ya Rais Samia nchini humo pamoja na yeye mwenyewe " sio jambo jepesi kwenda na muda mfupi huo huo ukapata pesa hii ni kazi kubwa hii, ni kazi nzuri ya mahusiano na kujitoa kwake Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan"

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amemshukuru Balozi wa Korea Kusini nchini Eunju Ahn kwa kuwa sehemu kubwa ya kusaidia kupatikana kwa miradi hiyo "nipende kumshukuru sana Balozi wa Korea Mheshimwa Ahn haya mafanikio tuliyioyapata nii kutokana na ushirikiano mkubwa huwezi ukafanya kazi peke yako"

Mradi huo utagharimu zaidi ya dola milioni 90 sawa na bilioni 170 mpaka utakapokamilika ambapo Waziri Aweso amesema itakuwa suluhisho kubwa kwa changamoto za maji katika hilo "kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa huduma ya maji safi na usafi wa mazingira kwa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam kutoka asilimia 45 ya sasa hadi asilimia 65"

IMG-20241216-WA1426.jpg

IMG-20241216-WA1423(1).jpg

IMG-20241216-WA1419(1).jpg
 

Attachments

  • IMG-20241216-WA1427.jpg
    IMG-20241216-WA1427.jpg
    105.1 KB · Views: 3
Upumbavu wa hali ya juu sana!

Baada ya zaidi ya miaka 60, chama kimoja kimeshindwa kufikisha hata asilimia 50 tu ya upatikanaji wa maji kwenye mji mmoja tu? Tena mji unaobeba taswira ya nchi!

  • Upatikanaji wa maji safi ya bomba umerudi nyuma kwa asilimia zaidi ya 30 kutoka 2021
  • Umeme imekuwa ni janga tena.
  • Huduma ya afya kapuni.
  • SGR haina hata mwaka, hali ni tete.
  • ATCL, ovyo!
  • TTCL, sijui ikoje hata!
  • Nguvu ya shilingi imeporomoka, tsh 10,000 si pesa tena, ni coin.
  • Unajenga BRT kwenye route inayopita daladala 100 kwa siku, hopeless.

  • Magari ya kifahari yameongezeka
  • Viongozi wa kisiasa na machawa wametajirika
  • Akina Godilavu wasio na jinsi ya upataji kipato ila wanachezea pesa mitandaoni wameibuka kwa wingi
  • Ubabe wa silaha umetaradadi
  • Vifo vya utekaji vinaongezeka kwa spidi ya mwanga.

Kubwa kuliko yote, DENI LA NCHI limekuwa kama mgomba ila halizai ndizi wananchi wanufaike...ingawa inasemekana kwa MKOLONI mambo si hapa siku hizi.

Tozo zinafanyiwa nini ikiwa imepita miaka na haijulikani kiasi gani kinakusanywa kupitia tozo zote zilizoanzishwa kwenye mawasiliano na mafuta ILIHALI shule hazina madawati wala barabara hatuzioni!

Maji, unaenda kukopa?
Yule mchina aliyesambaza mabomba miaka ile aliishia wapi?
 
Tokea tumeanzan kukopa au misada kwenye sekta ya maji, kila nyumba Tanzania ingekuwa na bomba la maji safi yasiyokatika.
 
Korea hii hii ambayo jeshi linaizingua serikali?
 
Watu hatuna maji week inaenda ya pili majamaa wanaleta hadithi za alfu lela ulela, bongo nyoso.
 
Hilo bango la mkuu wa mkoa linahusika vipi na utiaji saini wa huo mkataba wa maji taka?
 
Back
Top Bottom