kakamukubwa
JF-Expert Member
- Apr 23, 2012
- 203
- 27
Siku moja Tangu Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya viwanda na Biashara kusomwa Bungeni,Ni siku hiyo hiyo ndio Wizara ya viwanda kupitia chuo chao cha CBE,Kilitoa Barua kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na pili waliokuwa wakidhaminiwa na WIZARA HIYO kuwa kimesitisha UDHAMINI WAO KWA SABABU WIZARA HAINA FEDHA ZA KUWADHAMINI NA KUWATAKA WAENDE BODI YA MIKOPO kwa kuwa ahidi kuwasaidia.
Kwa Muhula wa kwanza mwaka wa kwanza mpaka wa tatu walipata fedha zao za kujikimu(1,480,000) na kuendelea na masomo,muhula wa pili MWAKA 3 na 2 NDIO waliopata stahili zao kidogo(230000),mwaka wa kwanza mpaka muda huu hawajapata stahili hizo kama hela ya chakula,malazi na kuwafanya waishi maisha magumu etc.
Fedha waliotakiwa kupewa na mdhamini wao WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA ni ya meal allowance=900,000,special faculty=156,000,medical allowance=200,000 Jumla 1,256,000
Nikiongea na Mmoja wa wanafunzi hao huku akikilaumu chuo kwa matumizi mabovu ya fedha ambayo CAG amebaini,alisema wao wanashangaa na kushtushwa taarifa ya kufutiwa udhamini huo ilihali WAZIRI WA VIWANDA DR ABDALA KIGODA,KATIBU MKUU BI JOYCE MAPUNJO,waliwaahidi kuwa ni lazima watamaliza chini ya udhamini wao kwakuwa ni sera ya wizara na Bunge ndilo liliopitisha na si mtu mmoja ILA kwa watakao anza mwaka huu hawatakuwa na udhamini huo.Iweje leo iwe hivyo? Kwa maana hiyo mwaka huu mwaka wa kwanza hawataenda kwenye mafunzo ya vitendo,ilihali mwaka wa pili nao wakiwa hawajui hatima ya fedha iliyobaki kama watapata na itawawezesha kwenda mafunzo ya vitendo.
Akiongea kwa masikitiko kuwa walichofanyiwa si kizuri ikiwa wao na watanzania na hawakustahili kufanyiwa kama walivyo fanyiwa? ina maana wizara inapenda watu waache kusoma,na kama wakiacha huo muda waliopoteza wataulipa na nini kwa sababu si wote wenye uwezo wa kujisomesha ni watoto wa masikini
Mwisho alimalizia kwa kusema watapenda kusikia kauli ya mwisho kutoka kwa waziri wa viwanda na BIASHARA ambae wana amini huenda akawa hajui chochote kuhusu kusitishwa kwa udhamini huo na kuongeza kuwa kuna wanafunzi walilipa ada ya muhula mwa kwanza ambayo mpaka sasa haijarudishwa na kusisitiza kuwa wanakidai chuo fedha hiyo kwa sababu wao walikuwa chini ya udhamini wa wizara ya viwanda na biashara kama wataicha huko ni kwamba mwakani watadaiwa ada ya muhula wa pili tu.
Nilimwuliza kabla sijaondoka je mko wangapi mliokuwa mnapata fund kutoka wizarani alijibu,
Mwaka wa 1 WAPO 21 wenye udhamini wa 100% WIZARA ni 14
Mwaka wa 2 wapo 38 wenye udhamini wa 100% wa WIZARA ni 22
Mwaka wa 3 wapo 16 wenye udhamini wa 100% wa WIZARA ni 14.
MADUDU YA CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA.
Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali amesema kwamba chuo cha Elimu ya Biashara kina usimamizi mbovu wa posho za kufundishia za wahadhiri na wakufunzi hali hiyofanya chuo hicho kulipa sh 74 mil zaidi ya bajeti ya chuo hicho iliyojiwekea mwaka 2011-2012.Bajeti ya chuo katika kipindi hicho ilikuwa ni kuwalipa wahadhiri hao posho ya kufundishia 300mil,lakini kutokana na usimamizi mbovu chuo kilifanya malipo ya sh 374mil.
CAG alisema CBE kiliwalipa wakufunzi kiasi cha sh 147mil kuanzia NOV 2011 Hadi JUN 2012 bila kuwa na mikataba na chuo hicho.
Chuo hicho pia kimetajwa kuwa na matumizi mabaya ya mishahara baada ya kuendelea kupokea kiasi cha 349mil kutoka hazina ikiwa ni mishahara ya watumishi 10 ambao walikuwa wamestaafu.Kati ya fedha hizo sh milioni moja ni mshahara wa mtumishi mmoja aliyekwisha fariki dunia.
CAG pia anaeleza katika ukaguzi wake amegundua kuwa MKURUGENZI RASMALI WATU wa CBE alikuwa ametimiza umri wa kustaafu tangu NOV 2008 ameendela kufanya kazi na kulipwa mshahara bila ya kuwa na BARUA ya ruksa kutoka kwa msajiri wa hazina.
Ukaguzi ulibaini watumishi watu waliokuwa wametimiza umri wa miaka 60 na kutakiwa kustaafu lakini wameendelea kufanya kazi na kulipwa mshahara.
madudu mengine ni chuo kutokuwa na idadi kamili ya wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho.