Wizara za Muungano.

Wizara za Muungano.

ZeMarcopolo

Platinum Member
Joined
May 11, 2008
Posts
14,040
Reaction score
7,303
Kuna swala moja linanitatiza. Naomba kushirikiana na wana JF kutafuta jibu lake. Katika mpangalio wa wizara Tanzania kuna wizara za aina mbili : wizara za Muungano na zile zisizo za muungano. Katika muundo wa serikali iliyopo sasa kuna wizara moja nyeti ya elimu na mafunzo ya ufundi. Hapo awali wizara ya elimu ya juu ilikuwa ni ya muungano na wizara ya elimu (ya msingi na sekondari pamoja na vyuo vya ualimu) ilikuwa si ya muungano. Sasa katika muundo huu unaounganisha wizara ya elimu ya juu na wizara ya elimu unaiweka wapi wizara hiyo katika muungona? Je ni wizara ya muungono au la?
Asanteni.
 
Back
Top Bottom