Wizi Chuo Kikuu Dodoma

Wizi Chuo Kikuu Dodoma

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Taarifa zilizotufikia ni kuwa kuna wizi (wenyewe huupamba kwa kuuita ufisadi) unaoendelea Chuo Kikuu Dodoma ambapo wanafunzi wanaohitimu wamekuwa hawarudishiwi pesa zao za kukodisha jofo kama yalivyo makubaliano na wizi huu umekuwa ukifanyika tangu mwaka 2011.

Utaratibu ni kuwa wahitimu hukodishiwa joho kwa gharama ya 50'000/= tsh, na kwa mujibu wa makubaliano kiasi cha 20'000 tsh hutakiwa kurejeshwa kwa mwananfunzi.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, wapo wanafunzi ambao huzungushwa kwa sababu kuwa fedha ziko utawala na mwisho huambulia patupu. Kama unavyojua, mwanafunzi anayehitimu huwa pale kwa muda mfupi tu baada ya mahafali kwisha hivyo muda wa kufatilia huwa mfupi na wengine hukata tamaa.

Mdau mwingine aliyesema nami alithibitisha kuwa yeye alirudishiwa, lakini alikiri kuwa kuna kundi kubwa kutoka Chuo cha Sayansi Asili na Mahesabu ambalo halikupata fedha kwa visingizio hivyo hivyo.

Hii si mara ya kwanza kwa Chuo hiki kikubwa kuhusishwa na wizi wa fedha za wanafunzi, miaka kadhaa nyuma kulikuwa na sakata la fedha za bima ya afya ambazo wanafunzi walilazimika kulipa huku huduma za matibabu katika zahanati ya chuo zikiwa za kusuasua.

Wasalaam!
 
Udom ni kitega uchumi cha vigogo,niliwahi kulipia provisional results na sikupewa, wala pesa sikurudishiwa. Joho nililipia, sikurudishiwa hata mia hadi sasa tangu 2012
 
mlipaswa kudai bila kikomo kuacha kwenu ndiyo kunawapa kiburi cha kuendelea kuwaiba!
 
Back
Top Bottom