Kuna changamoto ambazo hatuzielewi sisi kama wananchi kuhusu ukusanyaji wa Kodi ya jengo kupitia "Luku", na Mimi naomba kupata ufafanuzi Kwa msaada pia wa wananchi wengine, yaani mimi nimekuwa nikinunua umeme Kila mwezi, na wanakata wakati mwingine hadi 6000 eti ni deni la pango, lakini Cha kushangaza zaidi Kila mwezi wanakata ninaponunua umeme, na haijalishi umeme umenunua hata Kwa mwezi mara mbili, ila wanakata Kila unaponunua.
Zaidi Jana nanunua "LUKU" naambiwa deni langu ni kubwa, nikachukua jukumu la kupiga simu Tanesco, wakaniambia MITA yangu inadaiwa zaidi ya Tsh 20,000 na wakaniambia hawahusiki Kwa hilo, ila wahusika ni TRA lakini pia kupiga simu TRA nao wanasema hawahusiki, eti ni manispaa, na manispaa nawapigia simu nipate ufafanuzi namba naambiwa sio sahihi.
Hii inasikitisha sana Kwa wakazi wa Arusha jiji na maeneo mengine maana nimekutana na wafanyakazi wenzangu wengi wanalalamikia hii issue.
Ombi langu ni kwamba wakae chini wapitie mifumo yao, na waone shida Iko wapi, then watoe taarifa Kwa wananchi, yaani mtu una 10,000 unataka kununua umeme unapewa 2 units?
Na kama Kuna changes zozote ni kwa nini taarifa isitolewe?