Wizi kwa mawakala wa tigopesa - Mwazi akamatwa

Livia

Member
Joined
May 25, 2013
Posts
10
Reaction score
3
Tahadhari kwa mawakala wote wa Tigopesa

Wezi kwa kushirikiana na wafanyakazi wa tigopesa wamekuwa wakiwaibia mawakala wa tigopesa kila kukicha. Wiki iliyopita maeneo ya Kimara mtu mmoja kwa Jina la Ally Abdallah alikamatwa baada ya kutoa pesa kwa kutuma msg hewa. Msg huoneka imetoka tigopesa kama kawaida ila inakuwa na makosa mengi ikiwepo number ya simu ambao wanakutumia namba yako ya uwakala, pamoja na tarehe feki na salio feki. Mtu huyu kwa Jina la Ally Abdallah ni hatari sana na ameiba sehemu nyingi kama dodoma na kwingineko. Ukitafuta kwenye mtandao utamkuta ila inaonekana kote amefanikiwa kuachia na police. Mwezi huu aliiba maeneo ya Kimara na akakamatwa na kupewa mkong'oto wa kufa mtu. Alipotaka kuchomwa moto wasamaria wema walimtetea asiuwahe. Na alipopelekwa kituo cha police Kimara - wanamtandao wenzako walienda kumchomoa haraka na sasa ametoweka. Picha za kitambulisho chake hiki hapa. Kuweni makini huyu jamaa ni hatari sana. Anashirikiana na wafanyakazi wa tigo kuiba.
 
Wananchi siku hizi naona hawana HASIRA KALI, inakuwaje wamsamehe, TIA KIBERITI HUYO!
 
Huu wizi unaendelea kushamiri kwa sababu matapeli wanashirikiana na wafanyakazi wasiowaaminifu wa haya makampuni (tigopesa, m-pesa, airtel money etc)
 
You Guys nawasifu sana mana mnatusaidia sana wanajamii mana hapa umeokoa watanzania kama zaidi ya mia moja kwa hii habar peke yake.Thanx alot
 
Wajasiliamali wanajitahidi kujikwamua, wengine wanawarudisha nyuma. Balaa gani hili?
 
[h=2]Utapeli wa pesa kwa kutumia SMS washamiri[/h]
27/05/2013 NIPASHE: Mawakala wa biashara za pesa za mitandao ya simu za mikononi, wamelalamikia upotevu wa pesa baada ya matapeli wasiofahamika kuwaibia kwa kutumia ujumbe mfupi wa maneno (sms).

Wezi hao wanaodaiwa wanashirikiana na baadhi ya wafanyakazi wasio waadilifu wa kampuni za simu kuandaa na kutuma sms feki zinazowaibia mawakala mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Wakiongea na NIPASHE Jumapili (majina tunayo) mawakala walisema wizi huo umeshika kasi hivi karibuni na wengi

kupoteza mapato mengi. Walisema matapeli hao wanaofika kama wateja wengine hutuma sms wa kuhamisha fedha kwa wakala ukionyesha ametuma zaidi ya Sh 100,000. Wakala baada ya kuhakikisha sms hutoa fedha bila kujua kuwa ni utapeli.

Maeneo ambayo inadaiwa kukithiri kwa wizi huo ni Mwenge, maeneo ya Chuo Kikuu Dar es Salaam na katikati ya jiji: "Kutokana na ujanja huu tumeamua wateja wanaofika kuchukua fedha wanawasilisha vitambulisho," alisema mmoja wa wakala hao aliyeko Savei.

Walisema sms feki zinapoingia kwenye simu wanatoa fedha kwa mteja lakini salio haliongezeki na wanapochunguza wanabaini kuwa wametapeliwa na ujumbe feki. Wakifuatilia ujumbe huo unadaiwa hauonekani kwenye mtandao.

Walieleza kuwa biashara hiyo inaumizwa na matapeli kwa vile baadhi ya wateja wamesajili simu kwa majina feki na kuwasilisha barua za uthibitisho kutoka viongozi wa serikali za mitaa ambazo baadhi zimechakachuliwa.

Jeshi la Polisi lilipoulizwa juu ya madai hayo Msemaji wa taasisi hiyo Advera Senso alisema inawezekana mambo hayo yanafanyika na kuwataka wananchi kutoa taarifa sahihi za wizi wa sms. Alisema licha ya kuwepo wizi wa fedha kwenye mitandao ya simu na hata ya kompyuta wananchi wanatakiwa kuripoti polisi. Hata hivyo baadhi ya wafanyakazi wa kampuni za simu walisema wizi huo ni changamoto kwani baadhi ya matapeli wana utambulisho wa majina pekee kadhaa. Walisema tapeli anatumia majina zaidi ya 10 kwa vitambulisho tofauti hivyo kwa kutumia jina pekee huwezi kunaswa na kushauri alama za vidole na vitu vingine vitumike kusajili taarifa.




Source: Utapeli wa pesa kwa kutumia SMS washamiri - wavuti.com
 
Li mtu limeshiba kama mbunge wa ccm kumbe jizi, hivi huwa ananenepa na kuilea familia yake kwa huo wizi>
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…