Wizi kwa njia ya Mtandao, nini kifanyike kuudhibiti??

moshingi

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
278
Reaction score
93
Nimekuwa nikihuzunishwa na matukio mengi yanayoendelea kutokea kila siku kuhusiana na tatizo ambalo
limekuja pamoja na maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ambapo watu wengi hasa wenye kipato
kiduchu wamekuwa wakiibiwa fedha zao kutoka katika Akaunti zao za benki hasa NMB kupitia huduma yao
ya kuhamisha salio toka kwenye Akaunti ya benki kuzipeleka kwenye Akaunti ya simu za mkononi, kama vile M-PESA,
TIGO PESA na AIRTEL MONEY, au kutoka katika akaunti ya simu moja kwenda nyingine, vitendo hivi vimekuwa vikirudisha nyuma hali ya uchumi wa wananchi wengi wanaojaribu kujiwekea akiba zao katika mifumo hiyo ya uhifadhi wa fedha.
Hata hivyo kesi hizi zimekuwa hazipati mafanikio POLISI kwani kila mara utajibiwa kuwa bado tunasubiri majibu kuoka
AIRTEL au TIGO. Inachukua hadi miaka miwili bila kampuni hizo za simu hazijatoa majibu, je kama kampuni ya simu inamficha mtu aliyeniibia hela zangu kwenye akaunti yangu haistahili nayo kufikishwa POLISI?? Je benki ambayo niliweka
fedha zangu (hapa tatizo kubwa lipo NMB) nikiamini zitakuwa salama na kwamba mkataba wetu ni kwamba nitazichukua
fedha hizo pindi nitakapozihitaji lakini siku nakwenda kuchukua fedha zangu nakuta zimeibiwa kisha wananiambia nikaripoti POLISI je ni halali?? Wao si ndio waliokuwa na jukumu la kuzilinda hizo pesa kwanini ziibiwe zangu na zao zibaki?? Kwanini wao wasiende kuripoti POLISI ilihali wakiniachia pesa zangu nizitumie?? Tufanye kitu gani kuzilazimisha hizi taasisi ziache kutunyanyasa wanyonge??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…