Wizi kwenye mabenki nbc na zingine kwa kutumia master card

hahahaaaa basi safi,tukikutana tena, unitambulishe mkuu

Mkuu hebu niambie ni Benki gani nzuri katika hao washirika wa Umoja Switch? Hizi zingine naona sasa zinatishia usalama wa pesa zetu
 
Mkuu hebu niambie ni Benki gani nzuri katika hao washirika wa Umoja Switch? Hizi zingine naona sasa zinatishia uasalama wa pesa zetu

Ukiongelea huduma za ATM ukijiunga na benki yeyote ambayo ni member wetu utakua salama, ukijua hatua za kufata hakuna hata shilingi moja inaweza kupotea (labda uibiwe ATM card, na mara nyingi na mtu anayekufahamu na anajua PIN yako), tunaanza elimu kwa umma katikati ya mwezi ili wateja wetu wajue wapi pa kwenda inapotokea wamepata shida.

Ila unapokuja kwenye products nyingine hizi benki zinatofautiana sana, na zote zinashindana, mfano zipo zinatoa islamic banking zingine hazitoi, zipo zinatoa akaunti maalum za savings zingine hazitoi, rate za interest pia inatofautiana kutokana benki moja hadi ingine, sasa kushauri uende benki gani itategemea wewe unataka huduma gani.

 



Pole sana kwa rafiki yako, ila usikubali. Kuna wakati lilinitokea hilo na wakataka kunipotezea, hawakutaka hata nionane na bank manager. Nikawaambia nikitoka hapa naenda kwa waandishi wa habari, waliitafuta wenyewe hiyo hela wakairudisha. Mshauri aikubali mpaka wampe hela yake.
 
Mkuu asante. Nadhani suala la kutumia media linaweza kuwa zuri, kwa kuwa image yao itagundulika kirahisi. Kwa sasa nadhani wanawadharau wateja wao
 
Mkuu asante. Nadhani suala la kutumia media linaweza kuwa zuri, kwa kuwa image yao itagundulika kirahisi. Kwa sasa nadhani wanawadharau wateja wao

kutumia media ku-expose maujinga kama haya ni move nzuri sana!
 
kuna matatizo kwenye bank zetu na sisi wateja kama mnakumbuka kuna kipindi wabulgaria walikamatwa wakifanya wizi kwenye ATM walifikishwa mahakamani wakapewa dhamana na baadae wakatoroka sikusikia vyombo vya habari vikifatilia ,polisi walikuwa kimya na wale waliohusika na kuwapa dhamana walichukuliwa hatua gani?
nije kwa wateja wengi wanapopata matatizo wanakimbilia bank kumbuka huo uliofanyika ni wizi na wizi huo mara nyingi unahusisha wafanyakazi wa bank kwa hiyo unaporipoti bank wanachofanya ni kuharibu vielelezo ndio maana wanakwambia njoo baada ya si iku 45 ili baadae iwe rahisi kukukatisha tamaa.Nawashauri mnapopata tatizo hilo mbali na kutoa taarifa bank inabidi muwasiliane na bank kuu,mripoti polisi na pia waifungulie kesi bank husika kwani unapoweka pesa bank bank hiyo inapaswa kuhakikisha usalama wa pesa zako.
namshauri huyo mtu afungue kesi mahakamani pia awaombe wale wote waliopata tatizo kama lake wajitokeze ili waungane na kufungua mashitaka.
hakuna bank inayotaka kupoteza heshima yake kwa jamii ila jambo hili likiwekwa hadharani litawafanya watendaji wakuu wa bank washituke na kuchukua hatua kwani mara nyingi hayo mambo yanazimwa kabla hayajafika ngazi husika kwa hiyo tusiishie kulalamika bila kuchua hatua kwani hili tatizo limekuwa likijirudia bila kuchua hatua inabidi tulikomeshe kuna sheria za bank kuu,kuna sheria za polisi na kuna sheria za nchi tuzitumie
 
jamani naanza kuingiwa nawoga kuhusu hizi bank, hii taarifa ni mnzuri lakini jibu muafaka halijapatikana
 
[/QUOTE]

Mkuu Print out Bank Statement inakua na mtiririko wote wa Transactions coz hakuna m2 anaweza kutoa Pesa nje ya System.

Hata kama zile attachment zimepotea basi atapata taarifa yake ya fedha kwa kuprint Bank Statement anaanza upya kusotea pesa yake

Milioni mbili is not a JOKE
 

Jamani na mie nimeibiwa kwenye M-pesa kwa mtindo huu huu wakuingiziwa kwanza fedha laki moja then kesho yake nikakuta hazipo pamoja na balance yangu ya Tsh 100,000/=, nimewapigia Customer care wala sipati majibu mazuri toka kwao sasa naomba ushauri wa JF nifanye nini kupata haki yangu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…