Wizi mpya wa TANAPA

Eeka Mangi

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2008
Posts
3,173
Reaction score
482
Huu ni wizi mtupu!
Ninajua watu wa Kagasheki wanapita humu. Naomba mkamwambie.
Kila mahali sasa mnangáta bila kuangalia.
Miezi michache iliyopita Wizara ya maliasili na utalii ilituma pendekezo la kupanda kwa Tozo mbalimbali kwenye hifadhi zetu. Tour operator walipiga kelele sana kuhusu hili. Kama ilivyo ada Serekali sikivu ilisikia kilio cha tour operators! Kwenye pendekezo la awali pamoja na mambo mengine walipendekeza wahudumu kwenye hifadhi za taifa za Serengeti, Tarangire, Lake manyara, Arusha National Park ni USD 2 kwa trip kwa mhudumu mmoja. Hii inatoka tozo lile la USD 1 kwa kila mhudumu kwa safari nzima. Sasa serekali sikivu imesikia baada ya kupiga kelele na sasa itatoza shilingi 3500/ kwa siku! Huu ndio usikivu. Kwa hesabu za haraka mtu ataona kuwa ni sawa! SI SAWA hata kidogo! Huu ni wizi! Wizi mkubwa na unyonyaji a hali ya juu kwa wajasisiria mali wa kitanzania. Kwa mfano mpagazi anayepanda mlima kwa siku 7 atalipiwa shilingi 24500. Hii ina maana kuwa kuna tofauti ya shilingi 21000! Ukiwa na wapagazi 20 utalipa 490,000/ badala ya shilingi 70,000 tu! Tayari mjasiria mali huyu anatakiwa kuweka 420,000/ toka kwenye mfuko wake. Nasema mfuko wake kwa sababu takribani mwaka sasa tangu watoe pendekezo hilo tayari tour operator walishafanya agreement na agents wa nje ya nchi! Hhuu ndio usikivu wa serekali ya Tanzania.
Kama hatutasimama kuikemea serekali na serekali kusikia kwa maskio yake ya ukweli basi sio ajabu mkaona makubwa!
Tour operator wa Kitanzania chonde chonde simameni imara kupinga dhuluma hii. Kuburuzwa sasa iwe basi!
TANZANIA IS THE MOST EXPENSIVE DESTINATION IN THE WORLD! Like if you stands with me!
 
Hili jina la wapagazi silipendi. Acheni kulalama. lipeni hela
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…