Wizi na matumizi mabaya ya ofisi Hifadhi ya Ngorongoro

Wizi na matumizi mabaya ya ofisi Hifadhi ya Ngorongoro

BITALA

Member
Joined
Jan 10, 2015
Posts
26
Reaction score
26
Mheshimiwa Rais, Makamu na Waziri Mkuu shikamooni. Poleni na majukumu magumu ya ujenzi wa Taifa letu la Tanzania.

Ninawatakia mwaka mpya mwema mkiwa na afya njema.

Watanzania wenzangu habari za leo na poleni na majukumu ya kupambana na maisha.

Katika kumalizia mwaka naomba leo naomba kuwakumbushia kwa ufupi baadhi ya madudu kuhusu hifadhi ya Ngorongoro.

Kwanza niwape pole wahifadhi wachapa kaziwa ngorongoro kwa kifo cha faru fausta poleni sana na ninawatakia mapambano mema katika kuhifadhi maliasili zetu.

Katika kumalizia mwaka 2019 na kukaribisha mwaka 2020 naomba niweke kumbukumbu sawa kwa mambo yafuatayo yanayoendelea kwenye hifadhi ya Ngorongoro;

Uzembe na kutokuwajibika kwa ofisi ya Takukuru Lolilondo

Wafanyakazi wa taasisi hii kwa ofisi ya Loliondo hawamsadii Mheshimiwa Rais katika kuhaikiksha rasilimali za taifa hazitumiwi kijinga na watu waliopewa dhamana ya kuzisimamia.

Madudu yote yanaendelea kwenye taasisi hii wanayajua ila hawachukui hatua zaidi wamekuwa wakitumia ofisi yao kupata hela. Wamekuwa ni sehemu ya taasisi hii kwa kutokea kwenye kila vocha ya malipo sasa kwa mazingira hayo watawezaje kutimiza wajibu wao?

Nina taarifa mmeshaomba baadhi ya nyaraka zinazohusina na idara ya utawala kuhusiana na baadhi ya madudu yaliyofanywa na Ntunga na wasaidizi wake ili mfanye uchunguzi nawaasa fanyeni kazi yenu kwa weledi maana tuko tunawatizama kwa jicho la kikatili maana Ntunga na timu yake wanatamba wazi wazi nyie mnasumbuliwa na dhiki kwa hiyo watawapa hela na mtatulia so mjipange na muache tamaa mtafungwa.

Ninawashangaa mpaka leo watu manaowachunguza bado wapo kazini je hamuoni wanaweza haribu mwenendo mzima wa uchunguzi?

Je mmesahau Waziri Mkuu alivyokuja hifadhi ya ngorongoro mwaka 2016 alitoa maagizo kwa takukuru kwamba mtu anapokuwa anachunguzwa ni vyema awe amesimama kazi ili kutokuvuruga uchunguzi na mlimsimamisha kazi Bw Semfukwe kupisha uchunguzi je mnashindwaje kuwasimamisha hawa watumishi wa idara ya utawala kwa madudu waliyoyafanya wakati uchunguzi unafanyika?

Au ni hizo hongo mnazopewa ndo zinasababisha msichukue maamuzi?

Udhaifu wa menejimenti ya hifadhi kuchukua maamuzi bila upendeleo

Dr Manongi menejimenti yako haina msaada ikiwezekana ifutilie mbali, nilishawahi kukwambia na leo katika kumalizia mwaka nakukumbuha tena.

Hapo umezungukwa na wapiga dili ila sio watendaji wenye weledi. Ni jambo la aibu kwa kiongozi makini kusimama kifua mbele na kumtetea mfanyakazi aliyefanya makosa makubwa na akakiri yeye mwenyewe bila kulazimishwa.

Carlos Mbilo amefanya makosa makubwa sana kwenye ofisi ambayo ni very sensitive ila wako baadhi ya mameneja wanamteteta hivi nyie wapumbavu mna akili kweli. Mtu anayeweza kucheza na haki za wafanyakazi mnapata wapi ujasiri wa kumtetea?

Ina maana shirika halina watu wengine wa kuweza kufanya kazi zake? Si mmeajiri hivi karibuni wafanyakazi wapya wenye sifa na weledi Zaidi yake? Acheni kuwa na upendeleo kumbukeni anayeuwa kwa upanga na yeye kifo chake ni upanga.

Haiwezekani kijana huyu amefanya madudu hayo anapata ujasiri wa kutamba mbele ya wafanyakazi aliowaonea kwamba menejimenti haina cha kumfanya au ni Bangu unaamua kumtetea kwa sababu ulimtuma ukiogopa inaweza kutokea shida?

Kwa makosa aliyofanya nakukiri mbele ya kikao huyu anapaswa afukuzwe kazi sasa sisi tunausubiri huo uamuzi wa upendeleo mtakaouchukua.

Siku kumi n nne mlizotoa zimeshaisha ila vikao hamkai kutwa kukimbizana na hela as if Kreta itafukiwa haki ya Mungu tutawafunga kumbukeni Serikali hailali shauri yenu

Bangu umekuwa uanpenda kufanya kazi kwa mizuka hueleweki yaani unakuwa kama muimbaji wa singeli unaimba kulingana na kazi za mashabiki.

Umeshindwa kusimamia idara ya utumishi suala la mishahara na stahiki nyingine ni uozo uliopitiliza.

Baada ya kunusurika na kifungo umekuja na mikwara mingi ukaleta kamati toka utumishi haya mbona hatuoni hayo mabadiliko?

Bangu usitufanye sisi ni wapuuzi tunafahamu nyie ni timu moja mnatuchezea akili. Nashindwa kuelewa Dr Manongi unawezaje kufanya kazi na watu wapuuzi namna hii.

Bodi fukuzeni kazi hawa watu wasiotimiza wajibu wao mfano Ntunga sifa hana wakati wasaidizi wake wanazo. Idara hii isukwe upya haifai kabisa ukizingatia ndio imebeba maslahi ya wafanyakazi.

Tangazeni ajira wako watu wasomi wenye weledi watakaosaidia sababu kwa muda mrefu idara hii imekuwa ikihikiliwa na watu wasio makini angalau kidogo nasikia Bw.Mackiros alijaribu.Bangu unaacha kusimamia majukumu uliyoajiriwa kwa mujibu wa sheria unahangaika na yasiyokuhusu nakuhakikishia hili suala la mishahara litakupeleka jela ww kenua meno tu ukidhani uko salama.

Kilugha na Ntunga nawakumbusha fanyeni kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu hao wanajeshi mliowaleta na ambao mnalazimisha kuwapa majukumu ambayo hayapo kwenye muundo wa shirika mnajua impact yake?

Unamuandikia majukumu kwamba yeye ndo awe msimamizi wa wakuu wa kanda hicho cheo kipo wapi kwenye muundo wa shirika?

Mimi naendelea kuwaambia walikuwepo wababe kuliko ninyi leo hii wako mtaani wanahangaika sasa nyie endeleeni kudhani mko juu ya sheria mtaona yatakayowapata.

Idara ya ukaguzi wa ndani nawakumbusha mfanye kazi kwa mujibu wa sheria na taratibu

Msaidieni Dr Manongi acheni kulala mkidhani mambo yakiharibika mtabaki salama ninawaambia ukweli mtafungwa. Dhamana mliyopewa ni kubwa na uzuri uliopo sasa hivi mmekuwa wengi tena wa fani mbalimbali naomba sana timizeni wajibu wenu haya madudu yote ninayoyasema mlipaswa muwe mmeyaibua na kushauri hatua stahiki kuchukuliwa ili mnakaa kimya sababu nyie ni sehemu ya mfumo mbovu mnaofaidika nao.

Maleva umepoa sana kama uji wa mgonjwa yaani sioni makali yako kama mkaguzi mkuu wa ndani simamia vijana wako na usikubali upuuzi kama huo utokee.

Ntunga na Carlos wamekuwa na utaratibu wa kupokea hongo ya kuanzia milioni tatu mpaka nane ili kuwapa vijana ajira mpo mmekaa kimya.

Wako vijana wawili mmoja nayejulikana kwa jina la Hamis Mshana walioletwa na Carlos kutoka timu ya Geita Gold Mining anaoishi nao waliojariwa kwa cheti cha JKT na kuwaacha waliosoma wanyamapori wakati kipaumbele kilikuwa wanyama pori kwa kigezo ni wachezaji wazuri wa mpira mpo na mmekaa kimya.

Pitieni vyeti vya waajiriwa wapya kuna dalali za watu wenye vyeti feki walioajiriwa ili lisije likawaletea shida.

Maleva najua vikao vya maamuzi huwa unahudhuria na unaona kabisa wafanyakazi wanatumia vibaya nafasi zao mfano Ntunga, Carlos na wengine una rungu la kuijulisha bodi na kuchukua hatua stahiki hili la idara ya utumishi kuminya haki za wafanyakazi naona mnalipuuzia na kuona la kawaida ninawaambia halitawaacha salama.

Nyie sio watu wa mwisho msipoibua hoja za maana kulisaidia shirika na wafanyakazi wake sisi tutaibua na tutalianika hapa ili vyombo vya kiuchunguzi walifanyie kazi.

Edson Mwikemo mwaka mpya 2020 tunaenda kuunza nakuomba uache tabia yako mbaya ya kuomba rambirambi pale mtu anapofiwa maana ni laana mimi sijawahi onea mtu kama unabisha hujawahi omba rambirambi ili umsaidie mtu malipo yake kataa ili niweke ushahidi hapa.

Achana na tamaa sio kila hela ni ya kuitamani na ninawashauri hao NGOWWA watafute msaidizi wa Edson Mwikemo maana amekuwa kero muda mwingi hakai ofisini na wafanyakazi wanapofiwa akipigiwa simu hapokei sababu anajiona yeye ni untouchable shauri yako utarudi kwenu Tukuyu ukalime matembele.

Ila nina imani utabadilika na kuacha tabia mbovu zisizo za kiungwana.

Mwisho kabisa napenda kuwaasa wale wote wanaohangaika kujaribu kumtafuta anayeisadia Serikali kuanika maovu haya fanyeni kazi msijisumbue siko hapo kwa bahati mbaya mtapata taabu sana huo muda unamtumia kumtafuta Bitala utumieni kubadilisha mienendo yenu ya kiutumishi na kutenda haki la sivyo nitaendelea kuwaanika hapa na mtaangamia.

Uwezo wenu ni mdogo sana wa kuweza kupambana na mimi.Ninayafanya haya kwa mapenzi mema ya nchi yangu sababu shirika hilo ni mali ya watanzania wote na sio kikundi cha wapumbavu wachache wanaojiona wako juu ya sheria.

Kutokuandikwa kwenu ni kubadilika tu na kutenda haki la sivyo nitaendelea kutembea na ninyi kwenye suruali zenu mpaka kifo chenu japo najua wengi wenu safari yenu inaishia mwezi wa 4.

Nawatakia wale wafanyakazi watiifu wa hifadhi ya Ngorongoro na Watanzania wote kwa ujumla mwaka mpya mwema 2020.

Wabheja sana

BITALA
 
Wanasemaje hakuna awamu ambayo watu wanapiga madili Kama hii

Na hakuna awamu Deni la taifa limekuwa juu Kama hii

Na pia hakuna awamu yenye viongozi wanaoongoza kwa sifa ilhali hawana maarifa Kama hii

Na hakuna rais hapa amalizie Tundu Lissu
 
Mnazungukana tu....

Sio suala la ukabila ila hifadhi mmejazana wageni miaka na miaka na kazi ni majungu majungu tu toka enzi za mzee Msekwa. Wawekwe wenyeji nao waonje utamu wa aridhi yao.
 
Kwahio kungekua na makaburi wasingeondolewa au mm ndio sielewi 🤷
 
Back
Top Bottom