Abeid L Msanganzila
Senior Member
- Dec 30, 2018
- 163
- 343
Habari za jioni wana jf? Poleni na harakati za kutwa nzima.
Leo hii nimeamua kushare uizi mpya wa vifurushi vya internet nilioushuhudia kupitia kampuni ya VODACOM.
Jana jioni wakati nafanya jambo muhimu mtandaoni ghafla nikakuta simu imeganda kupakua files fulani, nikiangalia mtandao naona bado 4G inapepea, nikaamua kuangalia MB zilizobaki, nikakuta zimeisha.
Sasa nikaamua kuunga MB za jero ili nimalizie kupakua nyaraka zangu. Nikaenda menu yao ya JIMIXIE nikakuta 500=MB 285. Nikaunga, ila cha kushangaza nikapewa MB 110. nikahisi labda hizo ni za offer😂😂 kuangalia salio naziona zenyewe tu hakuna zingine. Nilipowasiliana nao wakadai nisubiri masaa 24. Sasa leo hii wamenijibu kirahisi tu eti tatizo langu limetatuliwa😂😂😂. Kiufupi wameniibia kihivyo wala hawajarudisha ata mia mbovu🤔,
Sasa wakuu, NAPE si huwa haamini kama tunaibiwa, na tayari nimeshaibiwa mm, nimewatumia maelezo hayo TCRA wapo kimya. Je nini kifanyike ili hawa jamaa wajue hela zinatafutwa wala haziibiwi au kuokotwa kokote!
Viambatanisho👇👇