wizi POSTA TZ

mama dunia

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2011
Posts
420
Reaction score
84
Naandika nikiwa nimeboreka na huduma za POSTA! mara nyingi naagiza vifurushi toka nje, na vinakuja kwa njia ya POSTA...bei ya huko vinakotumwa inakuwa ni nzuri ikiwa unatumia POSTA, ukitumia fedex na dhl inakuwa kubwa zaidi sana ya ulivyonunulia ndo maana ninaopt kutumia posta, lakini kweli maji yamenifika shingoni, yaani nimeshaibiwa mara 2! na kama mara kama mara 5 hivi ninakuta wamevifunguafungua sijui wanajua ninini kipo ndani humo! yaani wananiboa basi tu, huwa nawauliza kulikoni, utasikia na sie tumeletewa hivyo hivyo toka headquarter nk, nimeshatoa malalamiko hakuna kitu! njemba zinaendelea kufungua tu! sijui ndo kusema salary ndogo wanazopewa haziwatoshelezi ama vipi, mie wananiuzi sana, haya bwana ngoja nitafute njia nyingine rahisi ingawaje rahisi ni noma ila sasa kwa mie M-TZ bei sana inakuwa ngumu yani, maana unanunua kitu dola 50 utaletea dola 60 sasa hapo naona inakuwa ngumu,,,haya wadau ni hilo tu nimeona nishee nayi maana roho inauma
 
Mama Dunia hata mimi nimewahi kukutana na shida ya percel yangu huko posta. Nilikuta wameshaifungua na kuifunga tena, I was so furious! nilipouliza wakasema walikuwa eti wanakagua/wanaangalia usalama, nilijiuliza sikupata jibu yaani all the way from Ireland eti Arusha posta ndo wakague usalama, imagine? Kwa uzoefu ule sipendi tena kutumia huduma zao bora DHL
 
kweli yaani, mi nahisi mishahara haiwatoshi may be waongezewe,maana inakuwaje wale wa DHL/FEDX hawafungui? au ni maadili tu hakuna au tamaa tu, hata TTCL ndo wale wale, nimeomba simu miezi mi3 iliyopita kila ukiwambia vipi mbona hamji kuweka eti magari hamna ya kuja hapo hahahaha TZ noma sana
 

ni tamaa na kukosa maadili ya kazi. Wafundishwe ethics za kazi sasa.
 
pole sana. wa tz asilimia kama 70 ni wezi.kila mtu anaiba kulingana na wasaa wake.
 
Pole sana ndugu,haya mashirika yetu ya umma hayana tena uadilifu ni ufujaji kwa kwenda mbele.hapo kwenye nyekundu utumiaji wa hayo maneno naona sio sahihi kwa mfano "Kuboreka" lina maana ya kustawi ama imarika lakini sijui ulilitumia na kuchanganya lile neno la Kizungu "Bored" na kuliandika kiswahili kuonyesha umekata tamaa na huduma za hao jamaa wa posta ama la!
 

Duh hiyo hatali wanakagua usalama manually. Y wasiwe na scanner? Hata hivyo ni kazi ya airport au bandari wao wanascanner. Ni wezi tu hao
 
hahah si unajua tena ki-swanglish, halafu ukitoa kingereza kwenda kiswahili sometimes inakua ngumu kupata neno muafaka so ndo life linavyokwenda siku hizi, ila umenifurahisha kuiwakilisha BAKIATA hahaha

 
Wadau, poleni na kuwa bored.
naomba niwatetee posta kuhusu vifurushi kufunguliwa.
Vifurushi vyote vinavyotoka nje ya nchi ni LAZIMA vifunguliwe na watu wa customs kwa ajili ya ukaguzi. Hufanya hivi ili watoze kodi pale inapohitajika. Hili ufanyika airport.
Hata hivyo, watu wa customs wanawajibika kupiga muhuri unaothibitisha kuwa walifungua kifurushi hicho. Kwahiyo, kagua kifurushi kuthibitisha kama muhuri huo upo. Iwapo haupo, still usiwalaumu posta kwa sababu inawezekana watu wa customs (kama kawaida ya wabongo) hawajatimiza wajibu wao wa kupaiga muhuri.
 

Watanganyika bado tuko dunia ya kwetu, juzi niliposti parcel hapa UK , unaweza ukaitrack parcel yako lakini ikishaingia Bongo huwezi kuitrack nadhalni hata nchi nyingine za kiafrika ndio maana udokozi kama huo ni kawaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…