officialBossmtoto
JF-Expert Member
- Jul 1, 2019
- 370
- 1,189
Wanamaendeleo habari za leo
Leo naomba kuchangia mada na nyinyi kuhusu hawa ndugu zetu wanaojipatia kula yao ya kila siku na kuendesha familia kwa kutupeleka maeneo mbalimbali ya jiji. Mwanzoni Taxify na sasa ikifahamika kama Bolt imesaidia vijana wengi sana hasa ambao leseni zao zilikua zinatumika tu kama kitambulisho.
Balaa lililopo sasa tukiachilia mbali lile la zaman la kuendeshwa spidi ya 30 Km/h hata kama njia ni nyeupe ni hili la kuibiwa waziwazi.
Mara ya kwanza nilitoka msasani nikienda Airport nikalipishwa 65,000/- za kitanzania. Nilishangaa sana ila niliona kwa sim yake, yangu na mpaka Email ilisoma hivo. Basi nikalipa maana sikua na ujanja. Katika kuendelea kutumia tumia mara siku rafiki yangu ambae tulikua nae kwenye trip ya 65,000/- akanipigia na kuniambia ameshuhudia jamaa akiandika kwenye sim 10,000 na alivomaliza ikasoma 10,000 kote.
Yani ni kama app wameichokonoa au wana yakwao inayoingiliana na ya Bolt.
Hii ni ishara mbaya sana hasa ukishangaa hii Kampuni na zingine zimesaidia madereva tax wengi waliokua wanangoja abiria vijiweni.
Nawasilisha. Najua wapo watakaokuja na kusema kwamba suluhisho ni kununua usafiri binafsi, ila naamini wapo wenye usafiri wao ila kwa sababu za hapa na pale kuna mida inawalazim kuingia ubber ama Bolt
Sent from my iPhone using JamiiForums