Naomba kupata mchanganuo wa jinsi sheria inavyo weza kumlinda mwanachi wa kawaida kuhusu hili.
Makampuni ya simu yamekuwa yakifanya wizi ambao unaonekana wazi ama usumbufu ambao unawatia watu hasara kubwa pasipo kujali wala marejesho.
Mfano:Siku ya tarehe 12 nilijiunga na kifurushi cha Kabang toka mtandao wa tigo. Lakini mpaka leo hii hakuna huduma niliyopata wala refund. ni zaidi ya masaa 48-72, kwa ahadi zao wanasema tatizo linashughulikiwa ndani ya masaa 24. Lakini sivyo ilivyo katika hali halisi.
NOTE: Ni watanzania wengi wa wanakumbwa na aina hii ya wizi.mfano ni huu
Nchi hii ingeweza kuanzishwa upya ningeomba iwe hivyo,ukosefu wa maadili umeporomosha kila kitu,hii ndio maana ya nchi kutotawalika,dhuluma imekithiri,cha moto tunaendelea kukipata lakini kufa no.