Wizi wa kombe la dunia ulivyokuwa 1966, Westminster

Heri lee

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
981
Reaction score
537
Wakati tukielekea kwenye fainali za kombe la dunia zimesalia siku kadhaa leo tutajikumbusha mambo yaliowai kutokea miaka kadhaa iliopita juu ya kisa cha ‘’WIZI WA KOMBE LA DUNIA 1966’’
Wadau wa great thinker saloot kwenu
Hiki ni kisa cha wizi wakustaajabisha sana kwende pamoja

Mwaka 1966 Uingereza wakiwa ndio wenyeji na kufanikiwa kulitwaa kombe hilo mbele ya wajerumani 30 july 1966
Kombe la dunia lilirudishwa Jiji la London na kukaa jumba la makumbushao linaweka tunzo za kimataifa wanazochukuwa taifa hilo Westminster London.
Maafisa wawili waliokuwa on duty( katika kitengo siku hiyo) katika Hall la Westminster siku ya tukio Jumapili kipindi huduma ya kanisa la Methodis ikiendelea karibu na jengo hilo(WATU KATIKA JIMBO HILO WANAHESHIMU SANA TARATIBU ZA KANISA HILO) Hivyo walinzi pia walitakiwa kuhudhuria ibada siku hiyo huku ibada ikiendelea Wezi waliingia ndani ya jengo hilo wakiwa wakitumia ngazi walikuwa wameificha siku moja kabla wataalamu hao walikuwa wamejipanga maana walikuwa tayari wamechonga funguo zote na ramani ya jengo ilikuwa kichwani hivyo baada ya kuingia ndani walizima alarm systeam iliyokuwa imefungwa kwenye box la kioo lilikuwa limeweka kombe la dunia wezi walifungua lock na box hilo na kuiba kombe hilo
Taarifa za kuibiwa kwa kombe zilianza kusaambaa maeneo mbali mbali mwa jiji Vise Chairmain wa Football Association Coucil JACK STEWART alitoa maelezo kwa shirikisho la mpira wa miguu FIFA kuwa ‘’sisi ni wahusika wakuu hivyo tutawajibika kulitafuta hadi tulipate’’ we will responsible for find trophy he said
Utafutaji wa kikombe hicho ulidumu kwa siku nyingi bila mafanikio huku walinzi wa Hall la WESTMINSTER wakiwekewa kizuizi kuwa wanahusika wizi wa kombe
Mbwa alieitwa Pickles mmliki wake akiwa ni bwana David Corbett mkulima huyu alilipata kombe la dunia lililokuwa limefukiwa ardhini viunga vya jiji la London katika bustani ya maua Mbwa alinusa nusa kisha akaanza kufukua shimo huku bwana David akimwangalia Mbwa wake alishangaa kuona magazeti yamesokota kitu Fulani alipo yafungua alistuka kukuta ni kombe la dunia
Bwana David Corbett alikimbia haraka kituo cha ulinzi akisema “ I’m found the world cup trophy’’ nimepata kombe la dunia.Walinzi waliondoka nae huku wakidai anahusika na wizi lakini baada ya utafiti wakajua hahusiki na wizi Mbwa wa bwana David Corbett alikuwa maarufu sana hata leo alipewa zawadi ya mafupa makubwa yenye minofu ya bata na mmiliki wake akapewa hundi ya paundi mil 6000
Corbett alitumia hela kujenga nyumba kwa maana alikuwa hana. Mbwa alielipata kombe alifariki dunia na kuzikwa kifahari sana na juu ya kaburi wakalaza ubao uliondikwa “” Pickles the founder of world cup trophy""

Kwa kiufupi ndivyo ilivyokuwa lakini kombe hilo halitumiki tena baada shirikisho kutengeza kombe jipya lililoko hadi Leo
Ambao Germany ni watetezi

Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…