Wizi wa kura mfano wa historia ya James Meredith

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
WAMAREKANI LEO WAKIKUMBUKA MKASA WA JAMES MEREDITH WANATINGISHA KICHWA NASI TUTATINGISHA TUTAKAPOKUMBUKA NEC/ZEC NA WIZI WA KURA

Mississipi ni Kusini na Kusini ndiko kulikoshamiri utumwa wa mtu mweusi Marekani.

Ubaguzi ulikuwapo hadi miaka ya mwanzoni ya 1960.

Kuna sehemu Watu Weusi walikuwa hawarusiwi kwa ufupi mtu mweusi alionekana si binadamu.

Katika ubaguzi huu uliokubuhu kijana wa Kinegro kama watu weusi walivyoitwa siku zile akaomba kuingia kusoma Chuo Kikuu Cha Mississipi.

Kama ilivyotegemewa alikataliwa na hapa ndipo mkasa ulipoanza mahakamani na mahakama ikatoa.hukumu kuwa Meredith akubaliwe kujiunga.na chuo kwa ni kumkatalia kwa sababu ya rangi ya ngozi yake ni ubaguzi na kinyume ya katika ya nchi.

Kukifupisha kisa ni kuwa James Maredith ilibidi asindikizwe chuoni na kikosi cha jeshi na wabakie pale kumlinda hadi atakapomaliza masomo yake.

Katika sakata hili la serikali kulazimisha chuo kimpokee James Meredith watu walikufa na wengine kuumizwa vibaya.

Kisa cha James Meredith ni kisa maarufu katika historia ya ubaguzi Marekani.

Hii imebakia historia kwani Amerika ikaja kuchagua Mtu Mweusi kuwa Rais.

Kwenye mitandao kumejaa tuhuma za wizi wa kura mbele ya wale walioaminiwa kuhakikisha kuwa zoezi la kupiga kura linatekelezwa kwa haki na usawa.

Ukisoma na kuangalia matukio yanayodaiwa kuwa ni wizi wa kura na mengine yanayodaiwa kuvuruga zoezi lenyewe kuna maswali lukuki utajiuliza.

Hizi.kura za miujiza ndani ya viroba na mifuko nani anazitoa?

Nini makusudio yake?

Mbona na iweje wizi wa kura umefanywa kuwa jambo la kawaida Afrika?

Labda baada ya miaka mingi tutageuka nyuma na kutingisha kichwa na tutashangaa tutakapo kumbuka kuwa "kurafake," ilikuwa "order," maalum yetu wenyewe kwa ajili ya.kushinda uchaguzi.

"Kurafake," katika miaka hiyo ndiyo atakuwa James Meredith wao.

Wanafunzi watasoma katika somo la historia kuwa wizi wa kura ilikuwa mbinu muhimu ya kushinda uchaguzi.
 
Angalia picha:
Screenshot_20201028-232543.jpg
 
Hiki kisa cha James kizuri sana kukisoma. Infact hii ruling ya case ipo mtandaoni?
 
Back
Top Bottom