Elections 2010 Wizi wa Kura unafanyika hivi...

Duh.Hizi mbinu kali.Inabidi wananchi waamue kwelikweli,maana...............
 
Ni matumaini yangu jopo la wana CHADEMA ie Dr Slaa, Mbowe, Zitto, Marando nao wanaona haya tunayoyadiscuss.

Kwanza kabla ya kwenda kwenye uchaguzi Tume ya uchaguzi watuambie fika kuwa matokeo yatangazwe na kila kituo instantly, wapiga kura ni wangapi na vituo ni vingapi nchi nzima bila ayo mambo ni kheri wapinzani wakagomea uchaguzi
 
Kuyaona wanayaona, suala ni je wana resources za kutosha?? Financial na human resources itakuwa ni kitu crucial mno!!
 

Blue Monday lakini mkuu you made my Day. Kwakweli nimecheka sana.
Hii Habari nimeiamini 100% coz nilipata kuishi kule mara kipindi fulani.
Hawajamaa ndivyo walivyo. Hawana mzaha na haki yao.
 
Mnasahau mbinu moja ya serikali ya CCM ambayo niliwahi kuizungumzia humu miezi kadha iliyopita. Mbinu hii hushirikisha NEC. Mbinu hii pia imeripotiwa kutumiwa Ethiopia na Zimbabwe katika chaguzi zao.

Ni mbinu inayosababisha wapiga kura wengi wa upinzani kushindwa kupiga kura – kwa sababu ya kutaoyaona majina yao kwenye vituo vyao siku ya uchaguzi na kusababisha turnout kuwa ndogo kama ilivyokuwa hapa katika uchaguzi wa 2005.

Kwa mfano katika jimbo la Temeke ambalo ni ngome kubwa ya CUF – wapiga kura zaidi ya 100,000 hawakupiga kura mwaka 2005 kutokana na kutoyaona majina yao.

Kinachofanyika ni hiki: Hawa kumikumi (10-cell leaders) wa CCM hupita kila nyumba katika eneo lao na kukusanya majina ya wanachama wao waliojiandikisha kupiga kura pamoja na kuchukua namba za shahada zao za kupiga kura, na namba ya kituo (centre number). Nasikia kila mjumbe akikusanya na kuwasilisha majina 20 anapata Sh 50,000. Utaona basi kwa hali yetu ya umasikini, hii ni ajira kubwa ya kuishupalia.

Baada ya hapo, majina haya kutoka kila kituo hukusanywa pamoja na kupelekwa NEC ambako kazi yao kubwa ni ku-refer katika orodha ya wapiga kura katika vituo husika. Kazi ya NEC ni kuyaondoa majina ya wale wapiga kura wengine ambao hawamo katika orodha hizo zilizokusanywa na hao kumikumi wa CCM – yaani kubakiza wapiga kura wa CCM tu.

Majina ya wapiga kura wengine wote – ambao bila shaka watakuwa wa vyama vya upinzani -- ama hufutwa kabisa, ama huhamishwa kupelekwa vituo vingine ili wapiga kura husika wapate tabu kuyatafuta -- baada ya NEC kubandika hizo listi zao kwenye vituo wiki moja kabla ya uchaguzi.

Bila shaka kuna majina ya wapiga kura wachache wengine wa upinzani ambayo huachwa kama kudanganyisha tu.

Matokeo ya hujuma hii ni kwamba siku ya kupiga kura wafuasi wengi wa vyama vya upinzani hawayaoni majina yao katika vituo walikojiandikisha.

Na wale ambao waligundua kabla ya kupiga kura kwamba hayamo majina yao huwa wana muda mchache sana kurekebisha hali hiyo, hasa ukizingatia ile bureaucratic red tape ya NEC.

Nasema haya kwa sababu baada ya uchaguzi wa 2005, hapa Dar, mimi na rafiki zangu watatu tunaojuana hatukuyaona majina yetu katika kituo tulikojiandikisha – nasi wote siyo wafuasi wa CCM.

Wenzetu wawili waliyaona majina yao katika kituo kimoja huko katika kata ya Mchafukoge badala ya kituo chao walichojiandikishia. Mimi na mwenzangu mwingine hatukyaona majina yetu katika vituo vingine tulivyotembelea lakini bila shaka utakutwa yalipelekwa Manzese au Buguruni.

Lakini kuna hatari kubwa kwa CCM iwapo watatumia mbinu hii tena safari hii hasa kutokana na wafuasi wao wengi kukihama chama hicho na kuwa tayari kuwapigia kura wagombea wa upinzani, hasa baada ya zoezi lao la kura za maoni zilizojaa vurugu na uonezi.

CCM wanaweza kujikuta silaha yao inawageukia wao wenyewe…..

Aidha najaribu sana kutafakari hiyo hatua ya NEC kuyafuta majina zaidi ya milioni mbili kwa sababu waliyotoa ya kwamba wenyewe walikufa etc – as if hawakujiandikisha watu wengine waliotimiza umri wa miaka 18.

Inawezekana ni hao niliyosema hapo juu kwamba sasa wameondolewa kabisa katika orodha ya NEC?
 


Asante Mkuu kwa tahadhari hiyo: lakini itafikia wakati kwamba wapiga kura waige watu wa Tarime katika uchaguzi wao mdogo mwaka juzi. Wengi walikuta majina yao hayapo katika orodha ya wapiga kura vituoni na wasimamizi waliwaambia waondoke. Wakasema (huku wameshika sime) "Eti nini? Nisipige kura na hali shahada ninayo? Mwishowe NEC ilitoa agizo kwamba wote wenye shahada, hata kama majina yao hayamo kwenye orodha, mradi tu alikuwa amejiandikisha katika vituo husika, wapige kura. Chadema ikaibuka na ushindi! Laiti Busanda na Biharamulo wangewaiga watu wa Tarime, majimbo hayo yangekwenda Chadema.

CCM na NEC wizi sana wa kura hawa!!!!!!!!
Siku moja Watatutumbukiza katika vita.
 
taarifa nilizopata hivi karibuni kuwa badhi ya karatasi za kura za mwaka 2010 zitatengenezwa kwa teknolojia maalum ambapo kisanduku cha jk kitakuwa jirani kabisa na dr slaa, na mpiga kura akiweka alama ya kumchagua dr slaa inahamia kwa jk.

Karatasi hizi zitasambazwa katika maeneo ambayo inaonekana dhahiri dr slaa atashinda. Nasikia zinatengenezwa nchini vietnam
 
KUNA jambo moja muhimu sana:
Sitaki kupingana na mbinu ambazo wamekuwa wakizieleza waungwana kuhusiana na wizi wa kura kwa vile sina ushahidi nazo, lakini nataka kueleza kitu ambacho mie mwenyewe mimekiona na nina hakika hiki ndicho kinawaliza watu wengi sana mara baada ya kupiga kura.

Katika kampeni Vyama vya upinzani wamekuwa wakihamasisha watu kuwachukua wagombea wa CCM na kuwahukumu kwa kura, lakini wamekuwa wakishindwa kuwaeleza wapiga kura wao kuwa ni namna gani kura zinapaswa kupigwa.

KOSA lipo hapa:
Wanapokwenda kupiga KURA; Katika orodha ya wagombea 2 ama 3:
Mfano 1. Mgombea wa CHADEMA: M.M Mwanakijiji.
2. Mgombea wa CCM: Sikonge wa Sikonge.
Kwa haki wananchi wanakuwa wamemchoka mgombea wa CCM na wanamhitaji mgombea wa Chadema, lakini wakiingia katika sanduku la kupiga Kura wanaanza kumpigia wanaemtaka (Mgombea wao wa Chadema) wakimaliza hawatoki badala ya kuondoka kabla ya kukunja karatasi yao ya kura wanamtoboa MACHO ama kuandika maneno ya HATUKUTAKI/ HUFAI/ MWIZI n.k kwa mgombea wa CCM. Wakati wa zoezi la kuhesabu kura kura hizi nyingie zimekuwa zikionyesha kushinda lakini kwa utaratibu wa Uchaguzi kuwa na alama za Wino kwa maeneo yote mawili kura HUARIBIKA na hivyo mgombea waliyemtaka huanguka.

Hili lilitokea Geita, Kiukweli hawakuwa wakimtaka mgobea wa Ernest Mabina (CCM) na chaguo lao lilikuwa ni Malebo wa CUF, katika kituo kimoja cha kata ya Kamhanga kura ambazo Malebo alipigiwa lakini kwa mtimndo nilioueleza ziliharibika zilikuwa 68 hivyo Mabina wa CCM katika Kata hiyo alibakiwa na kura 145 kati ya 130 za Malebo na kama ungejumuisha na zile 68 basi ni wazi Malebo angeshinda. Hali ilikuwa karibu hivyo kila kata huku kata nyingine idadi ya kura zilizoharibika zikionekana kuharibika ikizidi kupanda mpaka 85.
Source: Frederick Katulanda wa Gazeti la Mwananchi
 

Kwa nini una-assume kuwa mpiga kura ndiye anayeharibu kura wala siyo hao wanaosimamia uchaguzi hasa baada ya kuona mgombea wa CCM anaelemewa na kuchukuwa hatua ya "kwenda chumba cha ndani ili kurekebisha mambo" kama alivyobainisha Baija Bolobi katika mchango wake #2 hapo juu? Wewe hushangai kuwa kura zilizoharibiwa (siyo sahihi kusema zilizoharibika) zote au kwa wingi ni zilizomchagua mgombea ASIYE wa CCM?

Hata hivyo shukrani kwa Mongoiwe kwa kuonyesha mbinu nyingine wanayotumia tri-angle ya NEC, Serikali na CCM, kuwaibia wapiga kura haki yao ya kuchagua viongozi wanaowataka.
 

Yap. Ni kweli kama masanduku hayatakuwa 'transparent' ni dhahiri kuwa kura zitaibiwa kama kawa. Muda wa kulipinga hilo ni huu na kama ikibidi uchaguzi uahirishwe mpaka suala la kutumia masanduku transparent LITAKAPOKUBALIWA
 
mimi nadhani kazi ni kwa vyama vya siasa kuhakikisha kabla ya uchaguzi vinapata idadi ya vituo vya wapiga kura vitakavyotumika na idadi ya watu kwa kila kituo ili kukitokea ongezeko la watu na vituo tume iueleze umma vimetoka wapi na orodha hii iwe wazi kwa watu wote tujue na iwe kabla ya uchaguzi
 



Mkuu hiyo tayari mwaka huu imeshafanyika shinyanga mwaka huu mwezi wa nane, nasikia kuna jamaa walikuwa wanadiscuss kwenye facebook wanasema ameshangaaa kuona mijitu inajifanya fundi bomba inawaeleza waananchi kuwapatia card zao za kupigia kura.

Yaani ni balaa.
 
Hii ni njia nzuri kwa kupambana na wizi wa kura!
 
ONYO lingine HAPA
Wakati wa kupiga kura kunapokamilika kunakuwaga na mchezo wa wasimamizi wa uchaguzi kuwagandisha kwa muda mawakala ili kuruhusu anayetaka kwenda kula akale. Hapo ndipo mtaona mawakala wa ccm wakijifanya wazalendo kuwasaidia mawakala wa vyama vingine kiuwezo ili wachepuke to lunch. Kosa hilo ni hasara kubwa kwani within short time chini ya uangalizi wa wanausalama kura huongezwa hata masanduku kubadilishwa ili wakati wa kuhesabu ukianza ionekane kura halali.

Dawa ni kwa mawakala kujitolea kutokula wala kunywa siku hiyo. Uzoefu huu niliupata ktk uchaguzi mdogo Temeke uliomweka Lyatonga bungeni.
 
Huu ndio uchakachuaji wa kura uliofanyika wakati wa kura za maoni za CCM. Lakini uchakachuaji huu bado athari zake zinaonekana mpaka leo. Kuna hali kubwa ya mpasuko haswa huko vijijini. Wanachama wa CCM wamekataa kata kata kushirikiana na wagombea "waliopita". Makundi ni mengi. Ni dhahiri kwamba ushindi wa kishindo HAUPO TENA kwa CCM mwaka huu. Wajiandae kwenda likizo, labda ya kudumu.

Somo: Usinyee kambi ungali mkazi.
 
Maalim Seif Shariff Hamad ametoa pendekezo la kupambana na wizi wa kura au namna ya kulinda kura.


Hizo bold ni msisitizo wangu.

Je, wasimamizi wa vituo watakubaliana na hilo? Je, kama chumba kina akina mama, itakuwaje? Suppose kama wakala ni mwanamama anaweza kutumia chupa?

NEC na ZEC mnatuumiza vichwa kwa vitu vidogo sana, kwanini mnasababisha yote haya? Mtakuja kuwafanya watu wafikirie hata yale ambayo hayawezekaniki. NEC na ZEC mnasikitisha sana, watendeeni haki wapiga kura, kwa kutimiza wajibu wenu bila kupendelea.

Yaliyotokea Kenya, hata Tanzania yanaweza kutokea. Jidanganyeni tu kwamba Tanzania bado ni kisiwa cha amani, nadhani rasha rasha mliziona siku ya uzinduzi wa kampeni ya CHADEMA pale mtangazaji wa TBC walipotaka kumshikisha adabu. Pia kura za maoni za CCM zitakuwa zimewaonyesha kwamba wananchi sasa wanajua haki zao.
 
Kinyume na watu wengi wanavyofikiria ni vigumu sana kuiba kura; chama kikiwa na usimamizi wa kutosha ni vigumu kuiba au kuweka kura za uongo. Kura zinaweza kuibwa pale ambapo tu vyama havijawaweka wasimamizi kabisa... au wameweka wasimamizi wenye kutafuta fedha tu.
 

Wakishindwa kuiba kura watapora tu ushindi kama walivyofanya Kibaki na Mugabe.....halafu watamwapisha JK haraka haraka tu hata iwe barabarani
 
Wakishindwa kuiba kura watapora tu ushindi kama walivyofanya Kibaki na Mugabe.....halafu watamwapisha JK haraka haraka tu hata iwe barabarani

Nyani.. watu wanaogopa tu.. sasa hivi tena NEC imebadili utaratibu wa kutangaza matokeo ya Urais kinyume na Kenya.. It is almost impossible to steal votes. Wengi wanaozungumza hawajui kura zinapigwa vipi, zinakusanywa vipi na zinahesabiwa vipi. Kuna utaratibu ambao ni very strict katika kuhakikisha matokeo ni yale ya waliopiga kura. Bahati nzuri nina uzoefu wa kuwa mmoja wa waaangalizi wa kupiga kura Tanzania na kuwemo kwenye chumba cha kupigia kura kuanzia asubuhi wanavyopiga kura hadi matangazo yanapotangazwa kituoni..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…