Elections 2010 Wizi wa Kura unafanyika hivi...


Kinadharia...tuseme imetokea Dkt.Slaa kapata kura nyingi kuliko Kikwete. Hivi kweli unataka kuniambia hakutakuwa na mizengwe ya kubadilisha matokeo? Yaani kweli CCM ita concede uraisi bila kupigana kufa na kupona? Ni vigumu sana mimi kuamini hii na nitaamini tu pale nitakapoona imetokea na imefanyika hivyo. Vinginevyo hadithi ni ile ile tu
 
Kinadharia...tuseme imetokea Dkt.Slaa kapata kura nyingi kuliko Kikwete. Hivi kweli unataka kuniambia hakutakuwa na mizengwe ya kubadilisha matokeo?

Nyani.. hivi unajua kura za Rais zinahesabiwa vipi? Chadema ikipoteza nafasi ya Urais lawama zitawaangukia Chadema na Chadema peke yao. Tusianze kutafuta kisingizio au sababu ya kudai kura zimeibiwa. Hoja hii naikataa mapema kama nilivyokataa Babati, Biharamulo na Busanda. Chadema wakitaka kushinda Urais mwaka huu wanaweza.. msisitizo uko kwenye neno "wakitaka".

Yaani kweli CCM ita concede uraisi bila kupigana kufa na kupona? Ni vigumu sana mimi kuamini hii na nitaamini tu pale nitakapoona imetokea na imefanyika hivyo. Vinginevyo hadithi ni ile ile tu

mzee ushindi wa asilimia 51 au 52 ni vigumu sana kwa CCM kuconcede. Chama chochote kitakachotaka kushinda uchaguzi wa Urais na kuing'oa CCM madarakani ni lazima kishinde kwa kile tunachokiita "a convincing majority yaani kuanzia asilimia kama 65 hivi kwenda juu..
 
Sasa wewe ndugu yangu,kama ulijua yote haya na una ushahidi kwanini ulikaa kimya siku zote?
Nina wasiwasi wewe pia ni mmoja wa hao wezi wa kura.
 
Mzee big up una data za kutosha. mimi biharamulo ni maskani na huyo mbunge unayemsema ni Oscar mukasa, yeye ni mganda kwa uraia lakini ndiye anayebebwa na ccm kwa sababu ni shemeji yake Makamba. Inauma lakini ni kweli, wananchi wameapa akipita asikanyage jimboni labada aje na walinzi.
 
Mbinu nyingine inayotumiwa ni kuwanunua mawakala wa vyama pinzani kwa kuwapa fedha nyingi kuliko posho kiduchu wanachopewa na vyama vyao..wakishanunuliwa inakuwa rahisi kubadilisha matokeo ya kura kwenye kituo na mawakala wanatia saini zao bila taabu kuhalalisha..si wameshapata cha juu wakati vyama vyao kutokana na ukata wanawashindisha njaa kutwa nzima ama kwa posho kiduchuuu!
 
Tujue kiini cha haya matatizo hata kwa kujitolea tukitaka mapinduzi ya kweli, baada ya hapo tujipange kutafuta ufumbuzi kuliko tuache kufuatilia ukweli na kubaki kulalamika tu.

Tujipange sawasawa, ukombozi u karibu kuja, hauji hivihivi,lazima tuufanyie kazi.
 
mzee ushindi wa asilimia 51 au 52 ni vigumu sana kwa CCM kuconcede. Chama chochote kitakachotaka kushinda uchaguzi wa Urais na kuing'oa CCM madarakani ni lazima kishinde kwa kile tunachokiita "a convincing majority yaani kuanzia asilimia kama 65 hivi kwenda juu..[/QUOTE said:
Heshima mbele MMKJJ: Unarudi palepale wanachozungumza akina Nyani. Kuto-concede in the face of slim defeat ni kuiba kura -- nothing else!
 
Katika nusa nusa kadudu flani kaniacha mbavu sina. Tofauti na ka-inzi kale huyu kadudu kakuta mijamaa flani wakibishania kura za ushindi wa Sisiem mwaka 2010. Sisiem tayari ina ushindi wa asilimia 80 na kwamba maboksi yalosheheni kura za ushindi huo tayari yapo kambi flani ya JeiWa baada ya kuwasilishwa toka China! Mmh!

Isitoshe, eti wale Wabongo waloandikisha laini zao za simu kwa kutumia vitambulisho vya kupiga kura wameingia mkenge kwani records zao tayari zinakuwa-processed pale kwenye mi-server ya NEC kuhakikisha ushindi kwa Sisiem asilimia 80!

Kali zaidi ni kwamba miboksi ya kupigia kura toka China ina uwezo wa kubadilisha TICK alopata mpinzani na kuweka pale kwa m-sisiem! Du! ?

Kazi kweli kweli! Huko Zenj, agents wa CUF vituoni tayari weshakumbushwa waende vituoni na chupa za ......... ili wasibanduke kabisa vituoni.!

Lisemwalo lipo?
 
Peleka umbea wako kwa shigongo.

... basi namplekea! naongeza dozi na kwamba imeagizwa MIGARI kibao ilosheheni maji ya upupu na full riot gear toka huko huko CHINA. tutegemee fujo baada ya sisem kupata asilimia 80%...
 

Mzee Mwanakijiji, zinduka usingizini. Hawa siyo wale waliosema hawawezi kuondolewa madarakani kwa vikaratasi? Wewe unadhani watasimama kimya tu na kuangalia wananchi wakiwaondoa madarakani kwa kura zao? Au una lengo la kuwasaidia kupumbaza wananchi ili wananchi wafikiri hii inawezekana, tena kwa urahisi tu?
 

Hizi zote ni mbinu za kuzubaisha. CCM huwa wana dummy votes zao ambazo hupigwa na kitengo chao cha Usalama wa Taifa. Hawa kazi yao ni kuhakikisha mgombea urais wa CCM anashinda.

Tanzania hatuna uchaguzi bali tuna uchafuzi, bila msukosuko tutapiga kura mpaka miaka 200 ijayo CCM itaendelea kujitangaza washindi. wanatumia uwoga wa wananchi kutimiza malengo yao. Zanzibar walimmwagia tindikali msimamizi wa uchaguzi mwaka 2000, siombi turudi huko ila CCM wanaoneka wanafanya betting kwenye maisha ya wananchi wakiwamo watendaji. Siku wananchi wakianza kuwaandamana watendaji kuwa ndiyo sababu ya wizi wa kura na kuhatarisha usalama wao sidhani kama CCM ina polisi wa kutosha kuwalinda watendaji wote.

Kuna jamaa yangu anatokea Ghana aliniambia kuwa kule uchaguzi ni satisfaction ya pande zote. Yaani upinzani unakuwa na tallies zake na chama tawala na msimamizi, baada ya hapo kinachofanyika ni kama "bank reconciliation statement", kwamba zikubaliane tallies za tume na ground records, na watu wapo makini kweli, Pindi udangayifu ukihisiwa tu ni kwamba uchaguzi umeharibika otherwise ni kuchapana. Tanzania tunahitaji system kama hii kwani ina faida zake.

1. Haiwapi guarantee watawala ya kurudi katika uchaguzi ujao hivyo kuwa makini katika kufanya kazi za wananchi na kuogopa wizi wa mali za umma kwani ukiiba kitu uchaguzi ujao ajaye anakushitaki.

2. Ina harakisha maendeleo ya wananchi kwa kuweka uwajibikaji kwani the ultimate decision of who will be coutry's leader rely on Public and not few individuals who can change electoral results to benefits their favourites.

Tanzania bado, tena bado but Iam betting on people who give up hopes for life because of poverty, there will be a time when they won't care being dead or alive, thata is where the justice will begin.
 
Hello,

Naomba nielekezwe jinsi ya kuweka poll

Title: Je, Fikra kuhusu wizi wa kura katika chaguzi mbalimbali nchini zina ukweli wowote?

1. Ndiyo, Zina ukweli

2. Hapana, Hazina Ukweli

3. Ni Hisia, ambazo haziwezi kuthibitishwa

Asante
 
Hello,

Naomba nielekezwe jinsi ya kuweka poll

Title: Je, Fikra kuhusu wizi wa kura katika chaguzi mbalimbali nchini zina ukweli wowote?

1. Ndiyo, Zina ukweli

2. Hapana, Hazina Ukweli

3. Ni Hisia, ambazo haziwezi kuthibitishwa

Asante

1. Ndiyo, Zina ukweli
 
Wapendwa sana wapenda demokrasia

NInawapeni pole kwa kipigo mlichopigwa na Real Enemies of DEmocracy in Tanzania (REDET) kwa kutangaza hadhdarani matokeo ya utafiti yaliyopikiwa pale Lumumba kwa uangalizi makini wa Dr. Makamba.

Mimi sijaja na hiyo hoja bali tunaangalia mbele namna ya kulinda kura kikamilifu zisiibiwe ama tupunguze sana wizi wa kura.

NImeweza kutengeneza documentary ya mafunzo ya WAJIBU WA WAKALA WA UCHAGUZI ambayo iko katika form ya DVD. Documentary hiyo ndio inatumiwa Ubungo, Mbeya Mjini, Hai, Bukoba na Mwanza. Ninawaomba sana wapendwa mnisaidie mambo matatu:-

  1. Wanaoweza kuifinyanga iingie huku by YuTube wanipe maelekezo tafadhali (0787 777790) na (0715 991150) hii DVD ina urefu wa dk 32 na ni ya GB 2.8.
  2. Ninaomba kila bidii ifanyike ili kila kata nakala ya DVD hii ama katika form ya VCD au VHS ifike itumike katika kuwafundisha MAWAKALA namna ya kulinda kura.
  3. Ninaomba wagombea wote wa ubunge na udiwani wafanye kila linalowezekana kupata nakala ya Mafunzo haya.
Ni imani yangu kuwa Wakala akiandaliwa vizuri akajua mbinu zilizoko katika chumba cha kura na namna CCM wanavyoiba kura kwa hakika lazima tutashinda.

NB: Pamoja na documentary hiyo ya video pia nimetengeneza brochure yenye maelezo
yote yaliyoko katika video husika. Imeambatanishwa hapa chini. Tafadhali fungua then print it out in landscape offcourse and the fold it at the middle to make it easy to carry.
 

Attachments

Heko Kamende

Asante kwa tool hii muhimu ingawaje imechelewa kidogo. Nami ninasisitiza kila mwanachama humu ndani atafute hiyo DVD na kuprint hii brochure. Nimeiona ilivyosheheni elimu ya kutosha kabisa kumwaandaa wakala akawa makini. Itabaki tu kuwaapisha wasihongeke.

Tafadhali mode msaidieni Kamende ili hiyo video ionekane humu.
 
mkuuu kamende unatisha unakubalika na una dhamira ya dhati nchi hii tutaikomboa tuu kwa kupeleka saana elimu ya uraia, kazi unayoifanya imekuja wakati maalum na muwafaka naomba copy kadhaaaa ziwafikie makao kuu ya chadema kila wilaya, lakini pia post hiyo DVD fasta, hii ni kuwaonesha we are beyond of what they think, mkuuuu umenifanya siku yangu ya leo iwe ya amani amaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii saaaaana lakin hili game bado mbichi saaaana jamaaaani pipo wake up, najua ccm wameingiza mamuluki ndani ya hii mitandao lakini uzuri ni kwamba kibaya cha jitembeza kizuri cha jiuza -big up Kamende.

ila sichelei kusema shame dr bannnnnnnwaaaa, shame prfo mwakandalaaaaa -get out of udsm we dont want to misuse our respected insitution for your personal benefits-where,
 
Tunahitaji wazalendo kama wewe mkuu. Mungu atakulipia
 
Mkuu Kamende naomba uniahidi kuwa nikiwasiliana nawe utanitumia kwa Basi ili niipokee hapa Morogoro... Nitaiduplicate na kuigawa (au kuipresent) kwa mawakala wote wa jimbo hili...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…