Elections 2010 Wizi wa Kura unafanyika hivi...


Asikubabaishe huyu Umar!
Huyu ni CCM kwa asilimia mia; na mdini wa kupindukia. Shwain
 

Sasa mimi nikifanya hayo na ninyi mliojipa hati miliki ya maoni na propaganda humu mtafanya kitu gani? Yaani ninyi mnataka kuondoa udikteta mmoja kwa kurasimisha udikteta mwengine, longolongo moja kwa kuhalalisha lonolongo jingine?

Nimeshasema kuwa I am craving for change but a reliable, efficient and responsible change....MBADALA MAKINI and what I see especially with the ongoing political trends, opportunistic and irresponsible campaigning, I only see BORA MBADALA tu na siko tayari kuconform na huo upepo wenu....

Just like nilivyokataa kubebwa na upepo wa MTANDAO 2005, ndiyo hivyo nakataa kubebwa na upepo wa UKOMBOZI 2010. Hiyo ni kwa sababu naamini watanzania we deserve and we can do better.....Hiyo ni kwa sababu I see hizi siasa kwa upana zaidi kuliko vichwa vya habari vya magazeti yetu na ushabiki wa jamiiforums...

Sasa kama wewe unaona hayo hayatoshi mimi kutokukubaliana na ukombozi wenu, well, fikiria unachofikiri....nimeyazoea hayo
 
Asikubabaishe huyu Umar! Huyu ni CCM kwa asilimia mia; na mdini wa kupindukia. Shwain

Asante Mungu akubariki wewe mzalendo na akuongezee utamu wa UKOMBOZI....Na kama kukaripia na kutokuacha wewe na wenzako humu kuendeleza chuki na kejeli dhidi ya imani na watanzania wengine wapatao milioni ishirini ndio sign ya udini wangu, well fikiria hivyo kwani mimi mwenyewe najijua na naamini katika misingi niliyoichagua na kamwe siwezi kubadili mtazamo wangu ili eti nimfurahishe mtu mwengine...
 
Thank you all for your useful input..........May the Almighty God bless all of us..............
 
umejikita kuwakosoa wale waliothubutu kufanya kitu bila kuonyesha wewe binafsi umefanya nini kurekebisha hali hiyo. Hivyo upo katika kundi la spectators ambao hukosoa maforward kwa kushindwa kufunga mabao. Tabia hiyo haiwezi kuchangia katika mabadiliko hata kidogo. Ni bora akina dr slaa ambao wamejitolea kuangusha mlima kidogo kidogo kulioka wewe unayekaa pembeni kuwakosoa walioanza kazi
 

ruta, ustaadh na wengineo kwanini hamtaki kuwa wakweli? Ni miaka mingapi wapinzani wamekuwa wakidai marekebisho ya katina, tume huru ya uchaguzi na kufutwa kwa sheria kandamizi? Na ccm inang'ang'ania status quo; kwa hiyo manataka kwa kuwa ccm inapendelea statu quo basi wapinzani wasuse kufanya kazi ya za kisiasa zinazowezekana kama vile kushiriki uchaguzi. Hali hiyo si itatoa kutoa mwanya kwa ccm kusajili vyama vibaraka ambavyo vitashiriki uchaguzi mkuu, na nchi hii kukosa kabisa anay trace of opposition. Kumbukeni ni kutokana na vyama vilivyopo kushiriki uchaguzi under protest ndio anagalau katika kipindi cha 2005-2010 raslimali zetu hususna madini vikapata waangalizi ndani ya bunge, kashafa za epa, richmond, meremeta mn.k vikaweza kushughulikiwa licha ya idadi ndogo ya wabunge wa kambi ya upinzani.

Na mwaka huu tunatarajia idadi hiyo kuongezeka kwa kuwa idadi kubwa ya wananccm pia inaonekana kutambua umuhimu wa upinzani katika nchi.

Rome was not built in a day; kadri wananccm na watanzania wengi zaidi wanavyochoshwa na ccm ndivyo idadi ya wabunge wa kambi ya upinzani itakavyokuwa ikongezeka, hatimaye tupate majority ya kutuwezesha kubadili katiba.

Acheni kuwakatisha wapenda mabadiliko tamaa. Hoja yenu ingekuwa na nguvu na mashiko kama baada ya ccm kutumia mapungufu yaliyopo kufanya vote rigging (kuiba kura) mgombea yeyote angehamasisha kuanzishwa kwa vurugu za kudai ushindi wake. Hapo sote tutamkumbusha kuwa you knew the rules of the game before entering the pitch.

Lakini mpaka sasa hoja yenu haina mashiko na tutaendele kuongozwa na mafanikio yaliyotokana na kambi ya upinzani katika bunge la 2005-2010 kuwaelimisha na kuwashawishi watanzania umuhimu wa mabadiliko kwa nia ya wapiga kura kutambua umuhimu wa kuwapatia kura wagombea wa vyama vya upinzania na kuwanyima kura wagombea wa ccm ili hatiamye one day tanzania iweze kupata katiba mpya kupitia bunge la jmahuri ya muungano wa tanzania.

 
Wakuu,
nimekuwa nikifuatilia pilika pilika za uchaguzi mkuu 2010 ambapo pamoja na mengineyo nimeshuhudia wagombea wakisisitiza wapiga kura kulinda kura zao baada ya zoezi la kupiga kura.


Kwa kuwa, kwa mtazamo wangu binafsi, jukumu la kulinda kura ni la wakala wa upigaji kura, kwani;
  • ndiye atakayekuwepo ndani ya chumba cha kupiga kura muda wote
  • atakatuwa wakala wa upigaji kura kwa chama husika
  • atakuwa wakala wa uhesabuji kura baada ya zoezi la kupiga kura kupita
  • atashiriki katika zoezi la kuhesabu kura
  • atatia saini kukubali matokeo ya upigaji kura kwa mujibu wa matokea halisi ya uhesabuji kura,

hatuoni kwamba zoezi la kulinda kura na wapiga kura litakuwa gumu sana kwa vile wakala wanaweza kushiriki katika kubadilisha matokeo baada ya kununuliwa?
 
na hata waibe hazitatosha...mwaka huu ni kuachana na hili dubwana CCM..wameshatuzingua sana
 
CCM wanaswa wakinunua shahada
• Wakutwa nazo 180 kibindoni

na Ali Lityawi, Bukombe



WAKATI juhudi za kuliokoa Jimbo la Bukombe ambalo liko katika hatihati za kunyakuliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) zikipamba moto, viongozi wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani humo wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa wakinunua shahada kutoka kwa wapiga kura.
Habari kutoka Bukombe ambazo zimethibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Selemani Nyakipande, zinasema viongozi hao ni Juma Mhoja na Shadrack Paul, ambao ni makatibu wa Tawi la Ushirombo na Msonga.
Alisema viongozi hao walikamatwa katika Kijiji cha Msonga, Kata ya Runzewe, wakiwa tayari wamenunua shahada 185 za kupigia kura kutoka kwa wananchi ambao walikuwa wanarubuniwa na baadhi ya makada wa CCM ambao wako katika mkakati wa kuliokoa jimbo hilo.
Viongozi hao walikuwa wakinunua shahada hizo kwa bei kati ya sh 2,000 na 5,000 huku lengo kuu likionekana kuwalenga zaidi wafuasi wa CHADEMA ili kudhoofisha nguvu iliyopo. Kamanda Nyakipande alisema polisi inaendelea kuwafanyia uchunguzi watuhumiwa hao kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwa madai kuwa tukio hilo linaingiliana na Sheria ya Gharama za uchaguzi. Hali ya kisiasa katika jimbo hilo ni tete kutokana na upinzani mkali uliopo kati ya CCM na CHADEMA, sababu kubwa ni kutokana na kuwapo makundi, baada ya kura za maoni zilizoibua malalamiko mengi
 
Jamani mimi nipo na problem sababu katika research zangu binafsi nimeona wazi kuwa jamaa watachemsha ila nipo pessimistic kuwa wata iba au lugha ile ngumu sijui kuchakakakaka...ua!sasa Chadema tumejipanga vipi kuprevent this!??:crying::crying::crying:
 
Unajua kuna watu wanachukuwa maoni ya watu karibu 20,000 hapa jamvini halafu wanayaapply kwa population ya zaidi ya watu milioni 40. I dont think it work like that.
 
Unajua kuna watu wanachukuwa maoni ya watu karibu 20,000 hapa jamvini halafu wanayaapply kwa population ya zaidi ya watu milioni 40. I dont think it work like that.

What do you mean emt!?? nimekuwa nikiongea na marafiki , majamaa na ndugu kuhusu huu uchaguzi na sikuangalia datas za JF nahh! lakini ukumbuke kuwa naweza kuwa wrong as hiyo ni my personal research sasa sijaifanyia proper methods za kiutaalamu either ni qualitative au quantitative! hapana mkuu! my personal conclusion! thanx!!
 
"The Legal and Human Rights Cente (LHRC) and a Tanzania Consortium on Citizen's
Election Observation (TACCEO) are involved in election observation using ICT.
Please be part by posting to 15540 any anomaly you observe during campaign,
voting, vote counting, vote tallying and results announcing."

Hii imetolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na Muungano wa Makundi ya Waangalizi wa Uchaguzi.

Hii hi Habari nyeti kwa Watanzania wote, watume message kwenda 15540 pale yeyote anapoona Kioja, Wizi wa Kura, Ufidhuli, au uharibifu wa makusudi kuharibu demokrasia na ushindi.

Tafadhali sambezeni hii kwa Blog zote, wapenda amani na kwa wapambanaji woooote!

Nawakilisha!!
 
Hii ni habari njema ingawa bado ninashaka na suala la ID ya mtoa taarifa
kama hapendi Id yake ijulikane, Kuna utaratibu gani uliowekwa?
 
Kwa habari kama hii basi tutarajie tarehe 31 mawasiliano ya simu na internet yatakuwa jammed mpaka hali iwe shwari. Quote this post
 
Nina wasiwasi kama hizo taarifa zitafika salama unaweza kukuta SMS zote zinakuwa monitored na UWT
 
Wana JF,

Nime pata tetesi kuwa kwa wale walio tumia vitamburisho vyao kwa kupigia katika zoezi la kusajiri namba zao katika makampuni ya simu nchini kuwa kuna uwezekano ndio njama ikatumika katika kuiba kura. Hiyo imebainika na mpenda maendeleo kutoka kwenye kampuni ya simu mojawapo nchini, CCM kuhusika na ilo jambo.

Nafuatilia kupata details kamili kuhusu hili, na kama kuna mtu pia nae huko afuatile kujua hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…