Geza Ulole
JF-Expert Member
- Oct 31, 2009
- 65,136
- 91,917
Ebu tujuze pls maana mimi ni mhanga
Thanks jethro... Usiishie kwenye tetesi, ukikamilisa urudi kusema
mamaa weeee.....sasa itakuwaje....mbona wahanga tupo wengi.....jamani chonde nyie wataalamu wa mambo haya mtuambie tufanyeje....na muda ndio huo unayoyoma
Wapinzani ambao mnahusika na usimamizi wa kura maeneo yenye vyuo vikuu, naomba muwe makini. Kuna tetesi kuwa cCM watapandikiza apiga kura wakitumia vitambulisho hewa na majina ya wanavyuo walioondoka maeneo hayo.
Wana JF;
Nimepata taarifa kutoka chanzo changu cha uhakika ndani ya Taasisi Nyeti inayofuatilia pia mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu 2010 ili kuhakikisha kuwa haki inatendeka na kuwa hakutakuwa na uchakachuaji. Hata hivyo Taasisi hiyo ambayo ni huru bado inaonekana imeshindwa kushughulikia kwa uhakika uchakachuaji unaondelea katika zoezi zima la uchaguzi ambalo bado linaendelea kugubikwa na vitendo vya rushwa na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.
Baada ya salamu za kawaida alinijulisha kuwa masikitiko makubwa kuwa Uchaguzi umepamba moto na kuwa mafisadi wamejiandaa kuiba kura "zetu" mpaka inakatisha tamaa.
Ili kupata uhakika zaidi nilitaka kujua wataibaje kura wakati NEC wamesema kuwa haiwezekani kura kuibiwa? Nilishangaa sana aliponijibu kwa kujiamini kuwa Niachane na NEC na kuniuliza nilitegemea NEC waseme nini? Akaniambia kuwa Slaa anatisha kwa "Wanachachama". alinihakikishia kuwa ikishindikana kabisa "watavuruga" uchaguzi kwa kuhakikisha kuwa vituo vingine vifaa havitafika.
Niliingiwa na wasiwasi kidogo na kumwuliza ni vipi hasa wataiba kura kwa maana nadharia hiyo mbona ni ngumu. Nilimwomba anieleze kwa uhakika. Akionyesha kujiamini na kuwa na uhakika na kile anachoongea aliniambia kuwa "Kwanza wananunua kadi za kupigia kura, pia kuna karatasi feki zimeandaliwa kwa ajili ya kuzidisha kura kwa CCM"
Habari ndo hiyo. Kama CHADEMA wanasoma hapa basi wajiandae kwa kulishughulikia hili.
Naomba kuwakilisha!
Wadau, hayo mambo ya kuiba kura CHADEMA wanayajua sana na kwa sasa wana uzoefu nayo wa miaka 10 au zaidi. Wamejifunza Tarime, Busanda, Ubungo na kwingineko. Napenda kuwatoa hofu kwamba mawakala wa CHADEMA wamekuwa wakipewa elimu ya jinsi ya kulinda kura kwa zaidi ya miezi sita iliyopita. Hii imefanyika kwa njia ya kuwagawia CD zilizorekodiwa maelekezo muhimu, semina elekezi na kadhalika.
Silaha kubwa ya Watanzania ni kupiga kura kwa wingi na bila kukatishwa tamaa na wasiwasi wa kuibiwa kura. Sheria ya Uchaguzi inaruhusu wapiga kura kukaa umbali wa mita mia moja toka katika kituo walichopigia kura wakisubiri matokeo ya kura hizo.
Tarehe 31 Octoba PIGA KURA, LINDA KURA YAKO!