Elections 2010 Wizi wa Kura unafanyika hivi...

Hapa kunauwezekano kweli kukawa na hizo kura feki, mfano kama watuwana kura feki akiingia nazo hapo si ndo utata hapo, tena anaingia naza urais ambayo ndo nyeti zaidi.
 
Nothig will work out!!!
 
Dah, niliutafuta sana huu waraka baada ya kufutwa ghafla, kweli wenye taarifa hebu wazirushe fasta hapa kitaani

 

Hii kali mpaka wahusika wakuu wanatajwa kwa majina? Hii taarifa inapashwa kupewa uzito unaostahili la sivyo haki haitatendeka hata kidogo!!!

Tiba
 
Wana JF Mnaikumbuka hii? Nadhani ilifutwa au kuhamishwa na Moderators lakini ilikuwa posted tarehe 10-10-2010. Bahati liliihamisha mapema kabla haijachakachuliwa!

 
Hii kali mpaka wahusika wakuu wanatajwa kwa majina? Hii taarifa inapashwa kupewa uzito unaostahili la sivyo haki haitatendeka hata kidogo!!!

Tiba


habari za CCM kuiba kura ziko wazi. Watu wengi wanafahamu. na kwanini huu waraka ulifutwa mbona hatukuelezwa? Mimi niliurudisha ukafutwa ghafla tena. kama ni makoza tuambiwe. Lakini Ukweli ndo huo
 

Hamna jipya uliloongea zaidi ya vile vile vilio visivyo na mashiko!!! Nilivutiwa kusoma thread yako hadi mwisho ili nione namna kura hizo zitakavyoibiwa lakini bado wala hamna kipya ulichosema!! Naomba unifahamishe yafuatayo:

  • Watanunua shahada ngapi hata waweze kuathiri matokeo ya uchaguzi?
  • Hizo karatasi feki zitaingizwa vipi kwenye masanduku wakati kuna mawakala wa CHADEMA? AU ndo tuseme kwamba mawakala wa CHADEMA watanunuliwa hata waweze kufunga mdomo? Na kama watanunuliwa, je unaweza kukiri hapa kwamba wana-CHADEMA ni watu wasioaminika kv ni rahisi kununulika kiasi cha kuuza haki ya Watanzania?
 

umri wako hauendani na mawazo yako, unawaza kizamani sana dogo, nakushangaa.
leo kwenu Temeke tumefanya kufuru pale Mwembe Yanga.
Kamwambia Makamba lile jimbo tunachukua.
 
leo katika shughuli yangu ya kuelimisha jamii huku shinyanga vijijini kuhusu umuhimu wa kupiga kura,tumetembelea kijiji kimoja kiitwacho ihalo.kama kawaida baada ya kutoa elimu kwa ile jamii tulikaribisha maswali au maoni au kama kuna yeyote aliyekuwa na dought.

ndipo aliposimama mwenyekiti wa kijiji hicho na kuanza kusema"uchaguzi uliopita katika kituo chetu cha kupigia kura wananchi wengi walikua chama cha upinzani na wengi walimpigia mbunge aliyekuwa angombea kwa ticket ya chama cha upinzani akiwemo huyo mbunge pia alijipigia kura ila cha kushangaza jioni wakati wa kuhesabu kura haikuwepo kura hata moja ya upinzani ikiwemo kura zote zilikuwa za ccm,sasa tulijiuliza hiyo mkura ya mgombea nayo ilienda wapi" ndipo walipotoa suluhisho kwamba hawako tayari kupiga kura kama ccm ndo wezi kiasi hicho,tumetumia kila njia kuwaelimisha na kuwahakikishia kuwa mwaka huu haitatokea wamekubali ila wengine kwa shingo upande,kwa kweli nimesikitika sana.
 
Akaniambia kuwa Slaa anatisha kwa "Wanachachama". alinihakikishia kuwa ikishindikana kabisa "watavuruga" uchaguzi kwa kuhakikisha kuwa vituo vingine vifaa havitafika.

Labda nikusaidie tu ya kuwa kuanzia sasa lolote CCM watakalolifanya litawaumiza wao wenyewe...........matakwa ya Mwenyezi Mungu kamwe hayawezi kubadilishwa na wanadamu hata siku moja......................
 
Kama inavyotarajiwa ushindi wa kiti cha "urahisi" utakwenda kwa JK. Dalili ziko wazi - sina hakika wanajamii wa JF mtaupokeaje ushindi huo! Tena wa kishindo - wenyewe wanavyosema!
 
Hakuna jipya kwa wapinzani Tanzania, tayari wamekwisha jiandaa na majibu yale yale ya 95' , 2000', 05' ila mwaka huu wana msemo mpya matokeo ''yamechakachuliwa''.
 
Kama inavyotarajiwa ushindi wa kiti cha "urahisi" utakwenda kwa JK. Dalili ziko wazi - sina hakika wanajamii wa JF mtaupokeaje ushindi huo! Tena wa kishindo - wenyewe wanavyosema!
Wenyewe wanavyosema tena!, sasa unataka tuwajibu hao wenyewe kwa kupitia wewe?. Waache hao wenyewe waje waseme wenyewe ili tuwajibu wao. Wewe nenda kalae ndugu yangu, mwaka huu mtoto si riziki!
 
Wana JF Mnaikumbuka hii? Nadhani ilifutwa au kuhamishwa na Moderators lakini ilikuwa posted tarehe 10-10-2010. Bahati liliihamisha mapema kabla haijachakachuliwa!

Mimi nimeambiwa njama za kuiba kura zipo na washirika wakuu ni watu wa Ikulu. Kuna kitengo maalumu kinafanya kazi ya kuiba kura kiko karibu na ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu. Kazi yao yote imekuwa ni kupanga njama za kuiba. Watu hao ni wa usalama wa Taifa. Wanashirikiana na mtu mmoja aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi lakni amerejea CCM. Kwa hiyo ndugu zangu tuhuma hizi si za kuupuza. Wao wana mpango wa kubadilisha idadi ya matokeo ya uchaguzi kutoka kila kituo kama alivyofanya Kibaki huko Kenya. Ninawahimiza Chadema walishughulikie hilo.
 
Ni kuhakikisha tu mabox ya kura yanakuwa mbele ya macho ya wakala wa chadema saa zote na hata ikibidi kulala zamu kuyalinda mabox hayo ili kulinda wizi usitokee basi ifanyike hivyo.
 
wewe mbona umeanza kulewa katikati ya wiki ikifika wkend itakuaje? nenda kapumzike unatuchafulia hali ya hewa,inaonekana uwezo wako wa kufikiri haupo sawasawa,we ni ndugu ya malaria sugu?
 
Kama inavyotarajiwa ushindi wa kiti cha "urahisi" utakwenda kwa JK. Dalili ziko wazi - sina hakika wanajamii wa JF mtaupokeaje ushindi huo! Tena wa kishindo - wenyewe wanavyosema!
Mpaka unasema hivi ni kuwa unafahamu rohoni kwako kuwa JK hastahili hata chembe kuendelea kuliongoza taifa hili na kwa hiyo ni ufisadi tu ndiyo utampa ushindi.......lakini hata NEC wakimtangaza mshindi unafikiri nchi hii ataitawala na wakati amekwisha kupoteza imani ya watanzania........Kule Mbeya msafara wake ulipigwa mawe......Mwanza leo kakumbana na zomeazomea....na mchezo bado..............Yaani hilo unalomwombea JK humpendi kabisa.....na haya niongeayo utayakumbuka hivi karibuni.........
 



Kaza buti siku tatu si haba utabadilisha wengi waliokata tamaa ya kupiga kura na kuibiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…