Uchaguzi 2020 Wizi wa kura za maoni katika mfumo mpya

Ndendende

Member
Joined
Oct 8, 2016
Posts
57
Reaction score
39
Walioshinda kwa kishindo wachunguzwe, majimbo ya Mtwara Vijijini na Nanyumbu. Mbinu ya kuwaandaa vijana maalumu ili wawasaidie wasiojua kusoma na kuandika imewapa ushindi wasiostahili.

Chama Cha Mapinduzi ifanye namna ya kuandaa utaratibu mpya wa kuweka sifa za kielimu hasa kwa wajumbe wanaotarajiwa kufanya maamuzi muhimu ya kumchagua mgombea katika kura za maoni within political part.

Hii ni kuepusha wabunge wajanja na wenye roho mbaya waache kabisa kutumia udhaifu wa wajumbe kutojua kusoma kuiba kura kwa kuwaandaa vijana ikiwa ni kinyume na utaratibu.

Mtwara Mjini Rushwa ilikuwa kama chai na hakika Takukuru kama wakishindwa kutoa taarifa kwa evidence basi tutakuwa tumemuangusha sana rais wetu Pombe Magufuli. Jimbo limekaa vibaya na aliyeongoza anajua kuwa haamini kilichotokea.
 
Walioshinda kwa kishindo wachunguzwe, majimbo ya Mtwara Vijijini na Nanyumbu. Mbinu ya kuwaandaa vijana maalumu ili wawasaidie wasiojua kusoma na kuandika imewapa ushindi wasiostahili.
Walifanyaje hao vijana na wasiojua kusoma
 
Kuna umuhimu wa kuweka elimu ya watu wazima kama kipaumbele hasa katika mikoa ya Kusini. Hawa watu hata kufungua account bank ni shida na hii ilipelekea kudhurumiwa mauzo yao ya korosho.
 
Elimu! Elimu! Utafiti wa 'Twaweza ' hatujausikia siku nyingi
 
Hivi miaka yote hii toka enzi za ngumbaru tumeshindwa kufuta ujinga wa kusoma na kuandika?

Kama hakuna tatizo katika mfumo wetu wa elimu basi kuna watu wanafaidika na ujinga watu kutojua kusoma wala kuandika.

Maadui: UJINGA, NJAA NA MARADHI NI MTAJI

Kwa jinsi hii; wapewa chumvi na fulana, wakata viunu na wapiga vigelegele hawataisha mtaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…