A
Anonymous
Guest
Kumekuwa na tabia ya utapeli wa kupangwa walengwa wakubwa wakiwa ni Mawakala wa huduma za kifedha haswa haswa wale ambao ni wapya katika eneo flani.
Limetokea tukio maeneo ya Sinza Mapambano ambalo ni muendelezo wa matukio ya utapeli, na cha kusikitisha licha ya kuwa na ushahidi wa picha na video za CCTV Camera, Polisi wanasema ni ngumu kuwakamata waharifu sababu ndo michezo yao.
Inasikitisha sana, kwamba licha ya ufumbuzi mkubwa wa teknolojia, Tanzania bado hatuna digital database ya waharifu wa namna hii na namna bora ya upelelezi na kuwatia mbaroni.
Watu wanarudisha nyuma sana kimaendeleo ya biashara.
Tukio tajwa linahusisha zaidi ya watu 3 ambao wote lengo lao ni kutapeli mawakala wa pesa kwa kujifanya wateja kumbe lengo ni kuwazubaisha mawakala na kisha kutoa pesa kwa njia ya kufoward message na sio kutoa pesa kwa njia halali kwa no ya wakala.
Hawa jamaa inaonekana wanazo taarifa za namba zote za mawakala wapya.