Jaman hebu tuelezane machache kuhusu huduma za hii benk yetu
kwa hapa magu Ukiweka pesa kwenye account isiyo yako ni lazma uambatanishe na shlng 1000/=,
je hii inafanyika hata wilaya zingine au huku MAGU wanaibiwa..!?
Mkuu kote nchini hata ARUSHA hilo tatizo lipo na hasa unapomtumia pesa mtu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.Lakini kwa taasisi za serikali mfano vyuo vya serikali na halmashauri hautozwi hela.
Waziri mkuu (mtoto wa mkulima) alishalitolea kauli hili kuwa wasiwatoze wateja wao buku,lakini wamedharau na kulikaidi agizo lake,sijui ilikuwa siasa!
Hawa ni wezi kweli, hivi haya mapato 1000/- huwa yanakatwa kodi? Wakati mwingine kwenye zile benki ambazo hazina kamera hawa tellers huwa wanachukua hizo buku buku zetu kwani hakuna monitoring ya kujua kuwa anayeweka ni mwenye akaunti au la, anayejua ni teller tu hivyo hata akila hakuna atakayejua na pia hizo gharama ni za nini maana hakuna tofauti mwenye akaunti anapoweka fedha kwenye akaunti yake na mtu mwingine anapoenda kumwekea. Kama tofauti ipo naombeni mnijulishe
crdb ya wapi?
Mkuu kote nchini hata ARUSHA hilo tatizo lipo na hasa unapomtumia pesa mtu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali.Lakini kwa taasisi za serikali mfano vyuo vya serikali na halmashauri hautozwi hela.
Waziri mkuu (mtoto wa mkulima) alishalitolea kauli hili kuwa wasiwatoze wateja wao buku,lakini wamedharau na kulikaidi agizo lake,sijui ilikuwa siasa!
Hii biashara ya buku buku ilishaondolewa toka tarehe 15 Jan 2012 tena walibandika tangazo walipobadilishabaadhi ya rate zao, hao mateller watakuwa wanakupiga mkuu nenda kwenye ubao wa matangazo utaona hilo tangazo.
Ebwana me nliwaona wezi eti ukiomba bank statement unakatwa buku, mbaya zaidi ni atm card, kama uko mbali na branch ulipofungulia hyo akaunt, kutumia atm card yako ni buku 15.