Wizi wa TRA kupitia kodi ya pango

Wizi wa TRA kupitia kodi ya pango

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kodi ni matoleo ya watu kutokea katika mapato yao ambayo kimsingi hayapaswi kuwa mzigo.

Mnapowalazimisha watu hata kwenda kukopa ili wawaletee tu nyie pesa kwa hakika hiyo siyo kodi tena bali ni wizi.

"Mtu kajenga nyumba yake kwa kujikongoja labda kwa miaka kadhaa ikimgharimu labda 60m/- + labda hata ni kupitia mkopo. Ile anapangisha tu, TRA hao mnadai 10% ya Kodi ya pango."

Hivi ni kwa mapato yapi hapo?

Huu siyo wizi? Halafu mnatokea hadharani bila aibu kudai mmevuka malengo?

Kwanini msiwe katika taasisi tarajiwa zitakazofumuliwa na kuwajibishwa panapo majaliwa, serikali ya watu yenye kuheshimu haki na usawa itakapopatikana?
 
wezi na dhuluma ndio maana nenda rudi tanzania haiendelei sio mji pekee hata watu wake sababu ya kudhulumiana
 
Zipo kero nyingi ambamo kupitia mikutano ya vyama vya siasa kwa kuweka misimamo yao kuhusiana na dhuluma kama hizi, wananchi na hasa waathirika watahitaji ufumbuzi kamili wala si maneno matupu.
 
Lakini kwa upande wa pili umejenga nyumba yako kwa 60 Million kwa miaka 10, sawa baadae unaamua kuipangisha kila mwezi laki 4 au 5 na kwa mwaka unapata milioni 4 mpaka 5 hii ina maana ndani ya miaka 10 milioni 60 yako imerudi sasa kwa nini usilipe kodi kwenye hiyo milioni 5 unayolipwa?
 
Umejenga nyumba yako 60m/- kwa mkopo wenye riba.

60m/- kwa maisha haya yenye ada hizi za shule, malipo kwa matibabu, bei za vyakula anazozishuhudia kila mtu, bei za petroli na dizeli, tozo mbali mbali kama zilivyo, nk nk, unadhani zinaokotwa kutoka wapi ndugu?

Kwa maana halisi hii ya TRA kudhani mtaji uliokotwa ni Kodi au ni wizi tu?
 
Kodi ni matoleo ya watu kutokea katika mapato yao ambayo kimsingi hayapaswi kuwa mzigo.

Mnapowalazimisha watu hata kwenda kukopa ili wawaletee tu nyie pesa kwa hakika hiyo siyo kodi tena bali ni wizi.

"Mtu kajenga nyumba yake kwa kujikongoja labda kwa miaka kadhaa ikimgharimu labda 60m/- + labda hata ni kupitia mkopo. Ile anapangisha tu, TRA hao mnadai 10% ya Kodi ya pango."

Hivi ni kwa mapato yapi hapo?

Huu siyo wizi? Halafu mnatokea hadharani bila aibu kudai mmevuka malengo?

Kwanini msiwe katika taasisi tarajiwa zitakazofumuliwa na kuwajibishwa panapo majaliwa, serikali ya watu yenye kuheshimu haki na usawa itakapopatikana?
brazaj. Shida siyo kwamba umejenga kwa ajili ya kukaa ni biashara tayari umefanya unataka kodi anai alipe?hapo hapo unategemea serikali ikuwekee ulinzi, unataka barabara nzuri,unataka uememe unadhani vyote vinakuja bure? unadhani sisi wa madukani ndiyo peke yetu tulipe kodi?kodi ushaambiwa ukifanya biashara,ukiajiriwa au ukiwekeza unalipa tu kodi.ushasema nyumba unapangisha huoni hiyo ni biashara? wewe lipa changia maendeleo ya nchi ndugu.
 
Usisahau nyumba zingine hizi tunapangisha baada ya kujikuta kuwa ends hazikutani tena. Wangapi wanaishia kupangisha nyumba ambazo hazikudhamiriwa kuwa za biashara?

Kodi haiwezi kutokuzingatia gharama za mtaji. Vinginevyo mapato yapi yanayoongelewa?
 
Lakini kwa upande wa pili umejenga nyumba yako kwa 60 Million kwa miaka 10, sawa baadae unaamua kuipangisha kila mwezi laki 4 au 5 na kwa mwaka unapata milioni 4 mpaka 5 hii ina maana ndani ya miaka 10 milioni 60 yako imerudi sasa kwa nini usilipe kodi kwenye hiyo milioni 5 unayolipwa?
je ile wanayokata kila mwezi unaponunua umeme sio ya jengo?
 
brazaj. Shida siyo kwamba umejenga kwa ajili ya kukaa ni biashara tayari umefanya unataka kodi anai alipe?hapo hapo unategemea serikali ikuwekee ulinzi, unataka barabara nzuri,unataka uememe unadhani vyote vinakuja bure? unadhani sisi wa madukani ndiyo peke yetu tulipe kodi?kodi ushaambiwa ukifanya biashara,ukiajiriwa au ukiwekeza unalipa tu kodi.ushasema nyumba unapangisha huoni hiyo ni biashara? wewe lipa changia maendeleo ya nchi ndugu.
Ni sawa na mimi napokea mshahara wangu kila mwezi lakini nakatwa PAYE.. Wewe ungesema si malipo ya kazi yangu niliyofanywa mwenyewe? Kwani TRA ilinisaidia kazini?
 
Back
Top Bottom