Mnasahau matumizi ya lugha kulingana na muktadha. Kimsingi magari husajiliwa kwa kupewa namba za utambulisho kwa madhumuni mbalimbali likiwemo suala la malipo ya kodi. Kwa hiyo pale gari linapoonekana limenominiwa WMN, JK, S, WM n.k ieleweke kimuktadha kwamba hizo ndiyo 'namba' zake. jambo hili lafanana kabisa na mnapokutana sehemu ya maakuli kama hotelini au mgahawani ambapo mhudumu hutokea akiwa amebeba oda nyingi na kuanza kuzisambaza kwa kuuliza: 'nani kuku?'. Na kwa hiyari yako mara zote umekuwa ukiitikia: 'mimi hapa'. Katika muktadha huu hatuwezi kuanza kukuita kuku licha ya ukweli kwamba ni wewe mwenyewe ulitutangazia kuwa wewe ni kuku!