WODI YA WAGONJWA MAHUTUTI (ICU) ILIYOJENGWA WILAYA YA IGUNGA - JIMBO LA IGUNGA
Wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU) iliyojengwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Hospitali ya Wilaya ya Igunga. Ujenzi umekamilika. Habari picha: Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe.
Nicholaus George Ngassa akipokea maelezo ya Wataalam wa Idara ya Afya kuhusu ujenzi wa Wodi ya Wagonjwa Mahututi (ICU).
Watanzania tusiendekeze bure kwa kila kitu, huu ni uvivu uliopitiliza, tukichangia ada ya matibabu kwa ajili ya kuleta mzunguko wa fedha katika hospital zetu hatutolalamika kukosekana kwa vifaa Tiba na dawa.
Uzuri wa gharama za matibabu katika taasisi za serikali sio kubwa kulinganisha na private or taasisi nyinginezo zote
Bora uende na kadi ya NMB na upate matibabu bora, Nilipata kutembelea mgonjwa alielazwa ICU ya Regional Referral Hospital moja ndani ya chumba kulikuwa hakuna mzunguko wa hewa kabisa kwani madirisha yalikuwa yamefungwa, unit ilikuwa inahudumiwa na ward attendant asiyekuwa na elimu yoyote ya ICU, pembeni ya mgonjwa kulikuwa na Portable ECG machine imewashwa lakini haipo connected kwa mgonjwa... Ilibidi niombe ruhusa kumtoa mgonjwa wangu mikononi mwa "Israel mtoa roho"