Wolper alia kutopata mtoto

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Super lady kunako tasnia ya sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ( 26), anadaiwa kuangua kilio kisa kutopata mtoto, Risasi Jumamosi limeinyaka.

Super lady kunako tasnia ya sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe, Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wake wa karibu, staa huyo amekuwa akihaha kusaka mtoto huku shinikizo likitoka kwa bibi yake, mzaa baba ambaye amekuwa akimuuliza juu ya yeye kumpata mtoto kwani umri unazidi kuyoyoma.

MADAKTARI WANASEMAJE?
Habari zilidai kwamba mwanadashosti huyo alishakwenda kwa madaktari mbalimbali ambao walimtaka kutokuwa na pupa kuhusiana na suala hilo na zaidi azidi kumuomba Mungu.

CHANZO CHATIRIRIKA
"Unajua umri ukishasogea , wanawake wengi huwa na wasiwasi juu ya suala hilo la kupata mtoto kama ilivyo ishu ya kusaka ndoa maana ni kati ya vitu vinavyowatesa. Jacqueline Wolper Massawe. "Wolper ana wataalam wake lakini hawajamwambia kama ana tatizo la kutopata mtoto . "Kuna maelekezo ambayo wamekuwa wakimpa ambayo humrejeshea furaha anapowaza ishu hiyo.

" HOFU TUPU !
"Madaktari walimwambia tatizo la kutopata ujauzito ina maana mwanaume na mwanamke au watu walio katika uhusiano wa kutafuta ujauzito ndani ya mwaka mmoja wameshajitahidi kufanya hivyo lakini wameshindwa . "Walimwambia pia inaweza ikawa zaidi ya mwaka mmoja lakini wastani kiwango cha chini ni mwaka mmoja ambacho Wolper alishakuwa na mwanaume lakini hakufanikiwa ndiyo maana wakati mwingine anakuwa na hofu . "Kuna wengine wanamwogopesha wanapomwambia kukosa mtoto ni tatizo kubwa katika jamii kwani kila mwanamke anataka afikie malengo ya kuwa na familia na hasa kunapokuwa na shinikizo la wazazi wanataka mjukuu .

TATIZO LIPO UPANDE WA PILI?
"Katika maelezo yao, madaktari walimwambia si mwanamke pekee anayeweza kuwa na tatizo bali hata mwanaume, hivyo tatizo linaweza kuwa kwa hao wanaume aliowahi kuchepuka nao , " chanzo kilimaliza kutiririka huku kikiomba hifadhi ya jina hadi atakaporudi mwana wa Adamu.

WOLPER APATIKANA
Baada ya kujazwa data hizo , gazeti hili lilimsaka Wolper ambapo alipopatikana, alifunguka kila kitu juu ya ishu hiyo.

BIBI YAKE KAMUONGEZEA MACHUNGU?
Akizungumza na gazeti hili mara tu baada ya kutua Dar kwa ndege akitokea mkoani Kilimanjaro ambako alikwenda kumsalimia bibi yake huko Old Moshi , staa huyo alisema kwamba hakuna siku ambayo aliumia kama alivyokwenda kijijini na kukutana na bibi yake na kuanza kumuuliza kuhusu lini atapata mtoto.

"Kiukweli hakuna kitu ambacho kiliniingia kwenye moyo kama bibi yangu kuniuliza kuhusu mtoto , nimejikuta nikitoa machozi tu . Ni kama alitonesha kidonda, " alisema mdada huyo.

Wolper alisema kuwa bibi yake alimsisitiza kwamba asijali kuhusu mtoto atakula nini bali akimpata ampeleke kwake kwani atakula chochote atakachokula bibi huyo . Katika maelezo mengine, Wolper alisema amejitahidi sana kutafuta mtoto lakini imeshindikana lakini anamuamini Mungu kuwa atampata kulingana na matakwa yake.

"Nimejitahidi sana kusaka mtoto lakini imeshindikana hivyo kwa wale ambao wanabahatika kupata mimba nawashauri wasitoe maana mtoto ni faraja kubwa kwa wanawake, " alisema Wolper.

CHANGAMOTO KUMPATA BABA BORA
Wolper aliongeza kwamba aliyachukua maneno ya bibi yake kwa mikono miwili na atayafanyia kazi, inawezakana mpaka mwakani anaweza kulikamilisha hilo lakini kuna changamoto moja tu anayokumbana nayo nayi ni nani wa kuzaa naye ambaye atakuwa baba bora wa mwanaye .

"Unajua unaweza kuzaa mtoto wala isiwe tabu kumlea kabisa kwani wapo watu wengi wanaweza kumwangalia, tatizo ni nani wa kuzaa naye tu jamani, " alisema Wolper huku akiamini kuwa siku ikifika Mungu atamjalia mtoto.

WALISHINDWA KUZAA NAYE?
Wolper aliwahi kuripotiwa kutoka kimapenzi na wanaume kadhaa wakiwemo mastaa wa Bongo Fleva , Ali Saleh Kiba , Nasibu Abdul ' Diamond Platnumz' , Khalid Juma ' Jux' na yule mwanaume aliyezua naye tafrani kabla ya kumwagana , Abdallah Mtoro ' Dallas ' na huyu wa sasa ambaye bado hajamuanika jina, wote eti wameshindwa kuzaa naye.
 
Hivi ukiwa bongo movie inatakiwa siku zote uwe na umri usiozidi miaka 26? Maana naona kila mwaka umri wao hausogei, kila mtu miaka hiyo hiyo duu
 
Ukiona amesema hayo jua kuwa hakuna mwanaume anayeweza kukataliwa kama akiamua kumtongoza wolper.
 
Mwambie aka asili mtoto kama madonna
 
Mmmhhh...anatafuta mtoto nje ya ndoa???si aolewe kwanza ndio aanze stor za kuzaa
 
Hayo ndiyo madhara ya utoaji mimba,unapotaka kuzaa inashindikana.
 
Angekuwa pure hata kidogo ningechepuka naye nimpe mimba hahaha!!
 
Aje nimpe hiyo kitu, tena kwetu tuna mbegu za mapacha
 
Hivi ukiwa bongo movie inatakiwa siku zote uwe na umri usiozidi miaka 26? Maana naona kila mwaka umri wao hausogei, kila mtu miaka hiyo hiyo duu

Ata mie nashangaa kujidogosha kwao sijui awatamani kuwa watu wazima daw!!

Hivi mtu asiyeolewa anaweza kusema amesaka mtotot mpaka akapata hofu? Alafu et ana miaka 26 hapo ndo wanajichanganya ina maana alianza kusaka na miaka 18 atleast ifike 10 ya kukosa matumaini.

Global muandeke habari zenye muktadha wa kiafrica single atatamani vipi kuzaa jamani?
 

Naunga mkono hoja kiongozi!
 
Naunga mkono hoja kiongozi!
Tena huyo bibi yake ndio nimeshindwa kumsoma kabisa (ikiwa global wanasema ukweli)anasisitiza mjukuwe agegeduke kwa bidii ili apate kitukuu?bibi kahaba kama mjukuu wake!
 
Tena huyo bibi yake ndio nimeshindwa kumsoma kabisa (ikiwa global wanasema ukweli)anasisitiza mjukuwe agegeduke kwa bidii ili apate kitukuu?bibi kahaba kama mjukuu wake!

Tatizo hawa wanaigiza hata katika maisha ya kawaida. Mwisho wake tutasikia wanaomba michango ya matibabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…