Wolper anyang’anywa gari

Chenge

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2011
Posts
1,073
Reaction score
377
Mwigizaji ‘five star’ kutoka tasnia ya filamu Bongo, Jacqueline Wolper Masawe, amenyang’anywa ‘mkoko’ (gari) wa kifahari aliokuwa akitanua nao katika mitaa ya mbalimbali ya jiji la Bongo.



Habari zenye ukweli 100% ambazo blog hi imezinyaka zinasomeka kuwa Wolper anayejulikana kama Amber Rose wa Bongo amenyang’anywa mkoko huo aina ya BMW X6 wenye thamani ya ‘ngawira’ za kibongo ML 170, sambamba na kupigwa ‘stop’ kukaribiana na mshefa aliyekuwa amemnunulia ndinga hiyo.


Kwa mujibu wa chanzo chetu, hatua ya mshefa huyo kuamua kuchukua ndinga yake ni baada ya kugundua kuwa Wolper anatoka kimapenzi na ‘sharobaro’ mmoja anayemiliki duka maarufu la viwalo pande za Kinondoni.


Aidha chanzo hicho, kimeieleza blog hii kuwa hivi sasa mwanadada huyo ameamua kutembelea ndinga aina ya Noah aliyokuwa anaitumia hapo awali sambamba na kutoka kwa kuvizia kukwepa watu wake wa karibu washitukie mchongo.

Katika kuhakikisha kuwa ukweli unajulikana blog hii iliamua kumsaka na baada ya kupatikana Wolper aligeuka mbongo na kudai kuwa hakuna jambo kama hilo isipokuwa kilichotokea ni kuwa gari limepata matatizo na ameamua kulipeleka ‘garage’.



Alipotakiwa kueleza kuwa imekuwaje gari mpya kama ile aipeleke garage tene kwa siku tatu Wolper alisme hivi:


“Bwana eeh wee jua liko ‘garage’ hayo maswali mengine mimi sitaki kuayasikia na kama una taka ugomvi endelea kuniuliza” alisema na kuondoka haraka eneo alilokuwa amekaa
 
Wasanii wa kibongo wana kazi sana.Alikuwa anamuhadaa nani sasa!!!! Ona sasa ameumbuka
 
Huyo mshefa nae ni mwehu tu. alidhani anaweza kufuga kunguru?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…